A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, January 3, 2022

Benki Ya Exim Yaendelea Kutangaza Washindi Wa Droo Ya ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’

 

.com/img/a/
Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Wateja wa benki ya Exim Bi. Agnes Kaganda, (Katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa zoezi la uendeshaji wa droo ya kuwatafuta washindi wa droo ya pili ya kampeni ya ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’ inayolenga kuhamasisha watanzania kujiwekea amana kupitia benki hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine ni ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bi Neema Tatock (Kulia) na Meneja Msaidizi wa Bidhaa za Rejareja kutoka benki hiyo, Callist Butunga (Kushoto)

Benki ya Exim imetangaza washindi wa droo ya pili ya kampeni ya ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’ inayoendeshwa na benki hiyo ikilenga kuhamasisha watanzania kujiwekea amana huku wakipata fursa za kunyakua zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu pamoja na gari aina Toyota Vanguard.

Akitangaza washindi wa droo hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Wateja wa benki ya Exim Bi. Agnes Kaganda, alisema jumla ya washindi 6 walipatikana kupitia droo hiyo na kujishindia zawadi ya shillingi million sita fedha taslimu.

Katika droo ya leo jumla ya washindi sita (6) wamepatikana ambao ni Manish Govindji, Abdulkarim Lema, Emashu Investment, Paul Kadonya, Emile Singano, Ibrahim Nyange na Pritipal Chadha na hivyo wameweza kujishindia zawadi za fedha taslimu kiasi cha sh mil 6.” alitaja

Washindi hawa sita kwa mujibu wa Bi Kaganda watakabidhiwa zawadi zao katika maeneo yao waliopo huku akibainisha kuwa benki hiyo itaendelea na droo kama hizi kila mwezi na washindi wataendelea kuingia kwenye droo itakayowawezesha kushinda zawadi kubwa ya gari aina ya Toyota Vanguard.

Wateja wetu wa sasa na wale wapya watakuwa kwenye nafasi ya kujishindia zawadi hizi kila watakapojiwekea akiba ya kuanzia Tsh. 500,000 na kuendelea. Kadili wanavyojiwekea amana kubwa zaidi ndivyo wanavyojiweka kwenye nafasi ya kushinda zawadi kubwa zaidi,’’ alisema Bi Kaganda wakati wa droo hiyo iliyohudhuriwa pia na muwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini.

Akifafanua zaidi kuhusu kampeni hiyo Bi Kaganda alisema inalenga kuleta mabadiliko kwenye mtazamo wa uhifadhi wa amana miongoni mwa watanzania kutoka kuhifadhi pesa majumbani na badala yake wazihifadhi kupitia benki hiyo kwa usalama wa fedha zao sambamba na faida nyingine nyingi ikiwemo riba.

Lengo si tu kuhamasisha watanzania kujenga utamaduni wa kujiwekea amana, tunachohitaji ni kuona kwamba Watanzania wengi wanajiwekea amana zao sehemu salama ili kujiendeleza kukua kiuchumi ndio maana tumejipanga kuwahamasisha watumie akaunti zetu mbalimbali ikiwemo akaunti ya mshahara inayotumika kwa matumizi mbalimbali ya kila siku,’’ alitaja.

Alitaja akaunti nyingine kuwa ni pamoja na akaunti ya mzalendo inayoendeshwa bila makato ya kila mwezi, akaunti ya haba na haba, akaunti ya faida ambayo inakuruhusu kuweka akiba na kupata riba pamoja na akaunti ya Nyota ambayo ni akaunti maalum kwa ajili ya Watoto pamoja na akaunti ya wajasiriamali inayowahudumia wafanyabiashara na mahitaji yao tofauti tofauti ya kibiashara.

Kwa upande wake Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bi Bi Neema Tatock alitoa pongezi kwa washindi wa promosheni hiyo huku akiwahamasisha walengwa kushiriki kwa wingi na kwamba wana nafasi kubwa ya kujishindia zawadi lukuki katika droo zinazofuata huku akiwahakikishia kuwa Bodi hiyo imejipanga kuhakikisha zoezi la kupata washindi linafanyika kwa kwa uwazi na kwa kufuata misingi halali ya kubahatisha.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages