KIKOSI cha Yanga SC kimesitisha kambi yake nchini Morocco kwa sababu zisizozuilika na kinaondoka leo kurejea nchini kupitia Dubai.
Lakini pia inaelezwa kuna wachezaji wamekutwa na maambukizi ya virusi vya corona na hao hawatarejea leo watabaki karantini kwa wiki moja.
Yanga ilikuwa imeweka kambi Jijini Marrakech nchini Morocco tangu Agosti 16 kujiandaa na msimu mpya na ilitarajiwa kurejea nchini Agosti 27, lakini kwa dharula iliyowakuta wamelazimika kusitisha kambi hiyo na kurejea leo.
Bado haijafahamika wachezaji watakaobaki Morocco ni akina nani.
No comments:
Post a Comment