MKURUGENZI wa Kivule Garden Wilaya ya Ilala ametoa eneo la kiwanja kwa ajili ya kujenga ofisi ya Tawi la SIMBA Kata ya Kivule Jimbo la Ukonga .
Akizungumza wakati wa kuzindua Tawi la SIMBA Kata ya Kivule Tarafa ya Ukonga jana Mkurugenzi wa Kivule Garden Joseph Luge alisema ametoa eneo hilo la kiwanja ili Tawi la SIMBA kivule wajenge ofisi ya kudumu waache changamoto ya kupanga na kulipa kodi.
Mkurugenzi Luge alisema hayo wakati wa chakula cha mchana eneo la Kivule Garden kilichoandaliwa na Mwenyekiti wa tawi la SIMBA Kivule Amos Hangaya mara baada ya kuzindua tawi la SIMBA.
"Uongozi wa Kivule Garden Wilaya Ilala umetoa eneo kwa ajili ya kujenga tawi la SIMBA itashirikiana na wanachama wa tawi la SIMBA Kivule katika shughuli zao mbalimbali zikiwemo za kijamii" alisema Joseph Luge.
Mwenyekiti Amos Hangaya alisema mikakati yao kujenga ofisi ya Tawi la SIMBA kivule katika eneo walilopewa na Mkurugenzi wa Kivule Garden kwa ajili ya wanachama wa Simba.
"Tunampongeza Mkurugenzi wa Kivule Garden kutupa eneo la kiwanja kwa ajili ofisi tunaanza mikakati yetu ya kwa ajili ofisi ya kudumu Kivule Wilaya ya Ilala" alisema Amos.
Mwenyekiti Amos Hangaya alisema mikakati yao mingine kufungua duka la SIMBA na kuuza vifaa vya michezo kivule .
Aidha alisema pia kuisaidia Serikali katika shughuli za kijamii kusaidia makundi Maalumu pamoja na Yatima ,Wazee Wasiojiweza sambamba na Wanachama kujiwezesha kujikwamua kiuchumi .
Katika shughuli hiyo ya kuzindua tawi la SIMBA Kivule pia Mwenyekiti Amos Hangaya alitumia fursa hiyo kuwaonyesha Wanachama wa Simba makombe yote ya ubingwa wa mwaka huu 2021 ambayo yalipiga PICHA nayo Kivule Garden.
No comments:
Post a Comment