KLABU ya Soka ya Simba leo imepokea kiasi cha Shilingi za Kitanzania Milioni 100 (Tsh. 100,000,000) kama pongezi na motisha kwao kutoka Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Sportpesa baada ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu wa 2020-2021 uliohotimishwa hivi karibuni.
Akizungumza wakati akikabidhi kitita hicho, Mkurugenzi wa Sportpesa, Abbas Tarimba amewapongeza Simba SC kutwaa Ubingwa huo msimu huu, Tarimba amesema Sportpesa imejisikia fahari kwa Klabu hiyo kufanya kile ambacho wamependa.
Amesema Sportpesa itaendelea kuwa na ushirikiano mzuri na Simba SC kama ilivyofanya ndani ya kipindi cha miaka minne ili kuhakikisha inafanya vizuri zaidi katika Mashindano mbalimbali Kama ilivyofanya msimu huu kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu kabla ya michezo yao kumalizika sambamba na kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Naamini malengo yetu yametimia kwa Simba SC kutokana na kufanya mambo mengi kwao, tunaamini bila Simba hakuna Yanga, bila Yanga hakuna Simba, hawa wote wanategemeana”, amesema Tarimba.
Pia Tarimba ameshauri Kampuni za Michezo ya Kubashiri kujitokeza kwa wingi kudhamini Klabu mbalimbali zinazoshiriki Ligi KuuSoka Tanzania ili kuleta changamoto kwa Klabu nyingine ambazo zinafanya vizuri katika Ligi hiyo.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez ameshukuru wa bonasi hiyo ya Fedha za Kitanzania Milioni 100 ambazo wamezipata baada ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu (VPL) msimu huu.
Amesema Soka la sasa linahitaji uwekezaji ili kupata mafanikio kuanzia Mashindano ya nyumbani, na hata Mashindano ya Afrika, “Tunashukuru Sportpesa wametudhamini vizuri kuanzia nje ya Uwanja na ndio maana tumejitahidi kufanya vizuri msimu huu.”
“Tunetimiza wajibu wetu msimu huu, tumeshinda Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Tumeshinda Kombe la Shirikisho (ASFC) na tumefika Robo Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ya CAF”, ameeleza Barbara.
Kwa niaba ya Wachezaji wenzake, Beki wa Timu hiyo, Gadiel Michael wameshukuru kwa bonasi hilo baada ya ushindi wa Ligi Kuu Tanzania, amesema wataendelea kupambana kuhakikisha wanafanya vizuri na mwenendo mzuri wa Mashindano mbalimbali ili kuendelea kufanya kazi na Wadhamini wao, Sportpesa.
Mkurugenzi wa Sportpesa, Abbas Tarimba akimkabidhi Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez na Mkurugenzi wa Sportpesa, Abbas Tarimba wakiwa wameshika kombe la ubingwa.
No comments:
Post a Comment