A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, July 25, 2021

HOSPITAL YA TMJ YAZINDUA MASHINE YA KISASA YA MRI WILAYA YA TEMEKE


Mkuregenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Mrisho Kikwete (JKCI), Prof. Mohamedi Janabi akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa wa Mashine ya kisasa ya MRI, ya Kwanza katika Wilaya ya Temeke—iliyopo katika Clinik Maalamu ya TMJ (Super Specialized PolyClinic) wengine ni Mkuu wa Wilatya ya Temeke Jokete Mwegelo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave,

Mkuregenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Mrisho Kikwete (JKCI), Prof. Mohamedi Janabi (wa tatu kushoto), akipata maelezo namna mashine hiyo inavyofanya kazi kutoka kwa wataalam wa hospital ya TMJ


Mkurugenzi Mkuu wa Hospital ya TMJ, Dtk Tayabali Jafferji, akiongea wakati wa uzinduzi wa Mashine ya kisasa ya MRI, ya Kwanza katika Wilaya ya Temeke—iliyopo katika Clinik Maalamu ya TMJ (Super Specialized PolyClinic). kulia ni Afisa Mtendaji wa TMJ, Bi Parul Chhaya , Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo, na mwisho ni Mkuregenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Kikwete (JKCI), Prof. Mohamedi Janabi. (Picha na Brian Peter) 

 Serikali imetoa wito kwa mashirika na kampuni binafsi za afya nchini kuwekeza katika miundo mbinu na teknoloji ili kuharakisha utekelezaji wa mikakati ya Kitaifa inayolenga kufikisha huduma za afya kwa mamilioni ya watanzania wahitaji, mpaka vijijini.

 

“Kuna watanzania wengi wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali ya afya, hasa maeneo ya pembezoni. Vituo vya afya na taasisi za Serikali, haziwezi kuwafikia watu wote hawa,” amesema Naibu Waziri wa Afya, Dtk Godwin Mollel, wakati wa hotuba yake ya Kuzindua mashine ya MRI katika Hospital ya TMJ.

 

Katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jayaka Kikwete (JKCI), Prof. Mohamed Janabi, Naibu Waziri amesema uwekezaji wa sekta binafsi katika teknolojia za kisasa za afya ni jambo muhimu litalosaidia Serikali kukabiliana na matatizo mengi ya afya yanayowakabili watanzania.

 

“Leo hii tunashuhudia TMJ wakizindua mashine ya MRI, ya kisasa, inayotumia teknolojia ya kiwango cha juu….nawahimiza wadau wengine wa afya kuwekeza katika teknolojia kama hizi ili kuwasaidia watanzania, ambao wengi wao ni maskini,” amesema Waziri Mollel wakati wa hafla ya uzinduzi wa MRI uliofanya katika Clinik Maalamu ya TMJ (Super Specialized PolyClinic) iliyopo wilaya Temeke-Dar es Salaam.

 

Amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa mashirika, makampuni na wadau wengine ya afya (kutoka ndani na nje) katika kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora za afya na zenye viwango.

 

“Nimeambiwa taasisi za afya zinakabiliwa na changamoto mbalimbali za kodi na nyinginezo…haya yote nimeyachukua, na tutayafanyia kazi, lengo likiwa ni kutoa unafuu kwa taasisi na kampuni binafsi za afya ili waweze kuwasaidia watu wetu,” ameongeza Waziri Mollel.

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TMJ Hospital, Dtk Tayabali Jafferji amesema uzinduzi wa machine ya kisasa ya upamaji wa magonjwa “MRI” ni sehemu ya mkakati wake wa muda mrefu wa kusaidia juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita zinazolenga kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.

 

“Serikali haiwezi kufanikiwa peke yake…sisi kama wadau wa afya (kwa umoja wetu) tunapaswa kutoa mchango wetu katika kufanikisha malengo ya serikali, hususani katika eneo hili la afya,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa TMJ.

 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa TMJ, hivi sasa dunia imekumbwa na milipuko ya magonjwa mengi tofautifauti, yanayotoka na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na staili ya maisha, mabadiliko ya tabia, ambayo matibabu yake yanahitaji teknolojia ya viwango vya juu sana.

 

Amesema kuwa Serikali peke yake haiwezi kukabiliana na milipuko ya majonjwa haya yote, na kuongeza kuwa sekta binafsi (taasisi na mashirika ya afya binafsi) yanapaswa kusaidia Serikali kwa kuwekeza katika mifumo na teknolojia ya kisasa itakayosaidia kuboresha utoaji wa huduma za afya.

 

“Hatua hii itatusaidia sisi (kama Taifa) kukabiliana na wimbi la milipuko ya magonjwa mengi (kama vile kifua kikuu na mengineyo),” amesema Dtk Jafferji, na kuongeza kuwa “Leo hii, sisi TMJ tunazindua mashine ya MRI, ya kisasa kabisa inayotumia teknolojia ya kiwango cha juu katika upimaji wa magonjwa mbalimbali. Na hii sehemu ya mchango wetu (kama taasisi ya afya binafsi) katika kusaidia Serikali kukabiliana na magonjwa mbalimbali, hivyo kuboresha utoaji wa huduma bora za afya kwa watanzania.”

 

Amesifu Serikali kwa kuweka mikakati dhabiti inayolenga kufikisha huduma za afya watu wengi, hususani mkakati mpya unakuja wa kutoa bima kwa watanzania wote, na kuongeza kuwa “hii ni hatua nzuri itakayowezesha watanzania wasio na uwezo kupata huduma za afya.”

 

Nae Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) TMJ, Bi Parul Chhaya amesema “Ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi za afya katika utekelezaji wa mpango wa Taifa wa bima ya afya kwa wote ni hatua kubwa na muhimu sana, ikaowezesha watanzania (kwa ujumla wake) kupata huduma bora za afya, bila kujali hadhi ya mtu.”






MATUKIO KATIKA PICHA





















No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages