A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, June 5, 2021

KAMPUNI YA UNILEVER TANZANIA YATOA MKONO WA SHUKRANI KATIKA HOSPITALI MBALIMBALI DAR ES SALAAM

 

Kampuni ya Unilever Tanzania katika kuendeleza ushiriki wake kwa jamii, imetoa mkono wa shukrani kwa wateja wake kwa kuzihudumia hospitali tatu za jijini Dar es Salaam ambazo ni Mwananyamala, Amana pamoja na Muhimbili.


Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutoa mkono wa shukrani, Meneja Masoko wa Unilever kupitia sabuni ya Omo nchini Tanzania, Bi Upendo Mkusa alisema, “Tunawashukuru sana Uongozi wa Hospitali n Wauguzi kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya na kuhakikisha mnaendelea kutoa huduma bila kuchoka, sambamba na hilo tunatoa pole kwa wagonjwa wote kwa changamoto ya afya wanayopitia, tukiwaombea kwa Mwenyezi Mungu mpate nafuu na kupona kabisa.


Mwezi huu tumeamua kutoa Mkono wa Shukrani kwa kutoa Shuka pamoja na Sabuni za Omo kwaajili ya kusaidia waliopo na kuhudumiwa katika hospitali hizi” aliendelea Bi Upendo.


Upendo alimaliza kwa kusema, “Tunashukuru sana kwa ushirikiano wenu kwani hali hii ndiyo inatupa motisha ya kuendelea kuwapa huduma bora zaidi. Ningependa pia kuwahakikishia kuwa tutaendelea kuwapa bidhaa bora na kuhakikisha tunatimiza mahitaji ya kila Mtanzania.

HABARI PICHA






No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages