Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL) imeendelea kutoa mchango wake katika kusaidia kuimarisha sekta ya kilimo nchini kwa kuwapa wanafunzi wa kilimo fursa ya mafunzo viwandani
Ikiwa ni muendelezo wa kuwapa fursa wanafunzi wa taaluma ya kilimo kujifunza kwa vitendo, kampuni hiyo ilitoa nafasi kwa wanafunzi wa chuo cha Kilimo na mifugo cha Kilacha Kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro kutembelea kiwanda chake kilichopo Moshi mjini.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti, alisema, “programu ya Kilimo-Viwanda inawajengea wanafunzi wa kilimo uwezo wa kuelewa kwa vimatendo. Kupitia ziara hii wanafunzi wameza kujionea namna malighafi za mashambani zinavyotumika kutengeneza bia’’.
Ocitti alifafanua kuwa ufadhili hchini ya Kilimo Viwanda unajumuisha malipo yote ya chuo na gharama zingine katika kipindi chote cha masomo kwa wanafunzi wanaochaguliwa na kuongeza kuwa programu hiyo inawalenga wanafunzi wanaotoka katika familia maskini ambazo haziwezi kumudu kugharamia masomo kwa Watoto wao.
Mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa program hiyo imelenga kusaidia juhudi za serikali kuongeza idadi ya maafisa kilimo. “SBL ni mzalishaji wa bia mkubwa nchini kwa kutumia nafaka za ndani katika utengenezaji wa bia. Hadi sasa SBL inafanya kazi na mtandao wa wakulima 400 kwenye mikoa nane nchini ambapo tunanunua nafaka kama shayiri, mahindi na mtama kwa ajili ya uzalishaji bia. SBL inatumia takribani tani 17,000 sawasawa na asilimia 70 na mahitaji yao kwa mwaka.,” alisema
Programu ya ufadhili wa masomo ya Kilimo Viwanda ilianzishwa mwaka 2020 na julma ya wanafunzi 71 wamenufaika nayo kwa kupata fursa ya kusomea kozi za diploma ya kilimo katika vyuo vingine vitatu ambavyo ni Kaole Wazazi College of Agriculture (Bagamoyo), cha Igabiro Training Institute of Agriculture (Bukoba) na St. Maria Goretti Agriculture Training Institute (Iringa).
Katika upande wake, meneja msaidizi wa chuo hicho, Padre Jerome Silayo aliipongeza kampuni ya bia ya SBL kwa msaada wao wa katika kusaidia maendeleo ya kilimo na kuyataka makampuni mengine kuiga mfano katika kuwasaidia wanafunzi kutoka familia masikini nchini.
No comments:
Post a Comment