WAZAZI wametakiwa kuweka ushirikiano na walimu wa wanafunzi ili kuongeza kasi ya ufaulu wa wanafunzi nchini.
Kuwapo kwa ushirikiano huo kumeelezwa kuwa kunasaidia kufuatilia mienendo ya wanafunzi na kuwaepusha na tabia za makundi rika na hivyo kuwafanya wajikite kwenye masomo.
Wito huo umetolewa Jijini Dar es Salaam na Mwasisi wa Shule Hurua ya Skillful Ukonga, Diodorus Tabaro, katika Mahafali ya 14 ya kidato cha sita.
Amesema ushirikiano utakaofanywa na wazazi kwa watoto wao wanaosoma kwa kiasi kikubwa utaweza kuwaongezea ufaulu.
"Shule yetu imekuwa ikimtengemea Mungu kwa mambo yote tunayoyafanya, hivyo nawahasa vijana hawa kuendelea kumtegemea Mungu wa kweli katika mitihani yao na kuamini wanafanya vizuri zaidi," amesema Tabaro.
Tabaro alisema shule yao imekuwa ikipokea wanafunzi ambao tayari wamekata tamaa na wengine wakuwa hawamalizi shule hivyo wamekuwa msaada mkubwa kwao katika utoaji wa elimu ambapo hadi sasa tayari wametoa wanafunzi waliomaliza vyuo vikuu mbalimbali wapatao 16.
"Unajua wanafunzi tunaowapokea ni wale waliokata tamaa ambao wengi wameishia njiani kimasomo na wengine waliokata tamaa baada ya kufeli darasa la saba basi tunawachukua na kuwapa mafunzo maalum ya kujitambua kwanza alafu ndio wanaanza kusoma masomo ya darasani na hii ili kuwafanya akili zao sasa kuchangamka katika suala la masomo," amesema.
Mgeni Rasmi ambaye ni Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu Dar es Salaam, Idara ya Sayansi ya Jamii, Dk. Simon Mtebi, aliwataka wanafunzi hao kuondoa hofu kipindi chote cha Mitihani na kuhakikisha wanamtanguliza Mungu.
Katika maafali hayo pia yalihudhuriwa na Msimamizi Mkuu wa shule zilizopo chini ya Taasisi ya elimu ya watu wazima, Baraka kionywaki.Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo ambaye ni Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu Dar es Salaam, Idara ya Sayansi ya Jamii, Dk. Simon Mtebi akizungumza na wahitimu pamoja na wazazi waliohudhuria.Baadhi ya wahitimu na wazazi wakimsikiliza Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo ambaye ni Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Idara ya Sayansi ya Jamii, Dk. Simon Mtebi. Mwasisi wa Shule Huria ya Skillful ya Ukonga, mkoani Dar es Salaam,Diodorus Tabaro akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mahafali ya 14 ya kidato cha sita.
No comments:
Post a Comment