Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Labour Party (TLP) Dominata Rwachungura (Pichani) akilaani vikali wanaobeza Msiba wa Rais.
Na: Richard Mrusha | Dar es Salaam | Chama Tanzania Labour Part(TLP) Kimelaani vikali baadhi ya Wanasiasa wanaobeza Msiba wa hayati Dkt John Pombe Magufuli kwa kutafuta majina kupitia msiba huu kwani inaonyesha ishara hata sifa ya kwa Raisi kuongoza hawafai kuwatumikia Wananchi na wawapuuze kabisa ni Wachochezi halitakii sifa Taifa la Tanzania.
Ameyasema hayo leo Mkoani Dar es salaam Mwenyekiti wa Chama hicho Dominata Rwechungura ambapo amesema Wakati Watanzania wakiwa na masikitiko makubwa kwa kupata pigo la kuondokewa na Raisi wao Mpendwa ambaye alikuwa mtetezi wa wanyonge Cha kushangaza watu wasio na Mapenzi mema na Nchi kutumia Mitandao ya kijamii kubeza inasikitisha Watanzania wawaepuke kabisa.
"Ni ukweli usiopingika ya kwamba Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania tumempoteza kiongozi tutakayekumukumbuka kujuta Mara kwa Mara kwa kwa Mambo yake mazuri aliyoyafanya kwa kuzuia rushwa, ufisadi, kuwatumbua wasiofanya kazi kupendana na kasi ya maendeleo bila ya pengo halitazibika na hatosahaulika" amesema Dominata.
Sanjari na hayo amesema TLP wanaamini Magufuli alikuwa mwalimu na Mfano mzuri wa kuigwa kiasi kwamba waliokuwa naye utawala wake wamejifunza kwake kwa hiyo tunategemea watajitahidi kutekeleza kwa kuendeleza yale Mambo mengi mazuri aliyotuachia katika nyanja wakati wa uhai wake.
"Kwa serikali ya CCM chama Cha Mapinduzi huu ni muda mgumu Sana kwenu ni wakati wa kuhitaji mshikamano mkubwa zaidi kilichobakia ni kumkabidhi MUNGU na kuwashirikisha Viongozi wa Taasisi zote za dini kushiriki katika Ibada ya kuombea Nchi yetu wakati huu wa maombolezo" amesema Dominata.
Sambamba na hayo Watanzania kushikamana na kusikiliza maelekezo kutoka serikali katika muda huo wa maombolezo kwa kusali Sana na kufuata maneno aliyokuwa anasisitiza wakati wa Uhai wake kumtanguliza Mungu kwa kila Jambo kwani yeye ni Muweza katika dhoruba Kali anatoa tumaini kwa wale wanaomtumaini kwa kupiga magoti kuelekeza kilio kwake kwa unyenyekevu na toba Kama alivyolisaidia Taifa kipindi Cha ugonjwa wa Corona.
Hata hivyo amesisitiza kwa kuwaasa Watanzania Makamu wetu wa Raisi ameapishwa kuwa Raisi kuongoza Nchi Mama Samia Suluhu Hassani kulingana na maelezo ya katiba ya Nchi Sura ya Pili ibara ya 37 kifungu Cha tano (5) Cha katika ameapishwa kuwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuchukua nafasi ya aliyekua Raisi Marehemu Dkt John Pombe Magufuli.
Pia alisisitiza Kama chama Cha TLP wamehakikisha kuwa hawana shida na uwezo wa Mama Samia Suluhu Hassani kuongoza watanzania hivyo asiwe na wasiwasi kwani katika uchaguzi Mkuu uliopita walimuunga mkono Raisi Magufuli wakati wa kugombea uraisi kutokana na uchapakazi wake ndiyo maana wawakuweka mgombea na yeye wanaimani naye.
Aidha Wito unaendelea kwa Watanzania kushikamana kuwa wamoja katika kipindi hiki kigumu kwani kazi ya Mungu haina makosa kila Jambo linakuja kwa wakati wake MUNGU atatushikilia atatupigania na kutupatia tumaini lililobora.
No comments:
Post a Comment