Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Mara
MGOMBEA ubunge katika Jimbo la Musoma Vijijini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Profesa Sospeter Muhongo ametaja sababu tatu kuu ambazo anazitumia kuwashawishi wananchi wa Mkoa wa Mara na Watanzania wamchague mgombea urais Dk.John Magufuli kuwa Rais kwa miaka mitano mingine.
Akizungumza mbele ya maelefu ya wananchi wa Mkoa wa Mara wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea urais uliofanyika leo Septemba 5,mwaka huu, Profesa Muhongo ametaja sababu ya kwanza ukienda duniani kote Rais anayependeka na serikali inayopendwa ni ile inayokuza uchumi.
”Hivyo sababu ya kwanza ni uchumi wetu,kwa miaka mingi umekuwa ukikua kati ya asilimia tano mpaka asilimia saba, ongezeko la Watanzania ni watu milioni 59.7. na thamani ya uchumi wetu ni Dola za Marekani 62.2 dola
”Kwa hiyo ukikagawa kwa kila Mtanzania halijavuka ongezeko letu la uchumi kati ya asilimia tano mpaka saba. Sababu ya kwanza ya kumchagua Rais Magufuli tuna uhakika uchumi unaendelea kukua kwa kasi kuwa kuliko ongezeko la watu,”amesema Profesa Muhongo.
Ametaja sababu ya pili ni ajira hasa kwa vijana, ajira zitapatikana kuendana na ukuaji wa uchumi,”Kwa kuwa uchumi wetu unakua kwa asilimia saba na umeshuka kwa asilimia tano, hata kwenye nchi nyingine zikiwemo za Marekani upo chini ya sifuri na sisi tuko juu ya tano
”Ilani hii ya uchaguzi mkuu mwaka 2020 ukiisoma inasema ongezeko la uchumi ifikie asilimia nane na watalaam wa uchumi duniani kote wanasema ukitaka kuondoa umasikini lazima uchumi uende juu kwa asilimia nane
”Tunaomba tumchague kwa kura nyingi, kule Musoma Vijijini nimefanya utafiti Dk.Magufuli anashinda kwa asilimia 98, kwa Mkoa wa Mara isiwe chini ya asilimia 95 na zaidi,”amesema Profesa Muhongo.
Ametaja sababu ya tatu inayosababisha kushawishi watanzania wamchague Dk.Magufuli ni ustawi wa jamii.”Na Taifa lolote lenye ustawi wa jamii na ndio maana unaona anafanya miradi mbalimbali ya maendeleo, katika ustawi wa jamii anastahili kwa mfano katika umeme jitihada nyingi zinafanyika.
”Bwawa la Mwalim Nyerere nilienda kule nikiwa Chuo Kikuu na sasa Rais Magufuli anajenga bwawa lile ili tuwe na umeme wa uhakika na utakuwa mwingi na hatutaumaliza.Reli ya umeme inahitaji huo umeme na bahati nzuri umeme wake hautavuka megwati 1000, tunataka uchumi uendelee kukuwa kwa asilimia nane, na bidhaa moja wapo ya kihistoria tutakayoanza kuuza umeme nje ya tanzania ni umeme.
”Hii sababu ya tatu ni sababu kubwa kweli kweli, ndio maana namuombea kura Dk.Magufuli.Na katika umeme tumeshaanza kuuza Kenya , tumejenga miundombinu ya kuuza umeme Zambia, sasa ndugu zangu wa Mkoa wa Mara, Ilani imetoka, hiyo Ilani tumeanza kuifanyia utekelezaji wake wa miaka mitano.
”Tunachosubiri ikifika Novemba 1 mwaka huu tuaanza kuitekeleza.Ilani iliyokwisha tuliongoza kwa Tanzania nzima kwa kuitekeleza na hii nayo tutakuwa wa kwanza kuitekeleza.Tumeandika vitabu viwili vya mafanikio,”amesema Profesa Muhongo.
Ameongeza katika jimbo lao la Musoma Vijijini waliomba barabara na tayari kilometa 40 zilishajengwa na hivyo wanaomba kilometa zilizobakia zijengwe na kwamba Rais Magufuli aliagiza halmashauri ya Musoma Vijijini ihame mjini na sasa wameshama ila ametoa ombi la kuhakikisha ofisi za halmashauri zinaikamilika.
”Ndugu zangu wa Mkoa wa Mara kuna mengi yamefanyika na hivyo tumchague tena Dk.Magufuli ili aweze kuendelea kuueleta mkoa wetu maendeleo,”amesema Profesa Muhongo.
Wagombea nafasi za udiwani katika mbalimbali mkoa wa Mara wakihamasishana kupiga push-up kuonesha uimara mbele ya Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala Rais Dkt John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni katika uwanja wa Mkendo mjini Musoma mkoa wa Mara leo Jumamosi Septemba 5, 2020
Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere akiwasili na wanae Makongoro na Madaraka Nyerere kujiunga na wananchi wa mkoa wa Mara kumsikiliza Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala Rais Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni katika uwanja wa Mkendo mjiniMusoma mkoa wa Mara leo Jumamosi Septemba 5, 2020
Mama Janeth Magufuli akimwamkia Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere alipowasili kujiunga na wananchi wa mkoa wa Mara kumsikiliza Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chamahicho Tawala Rais Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni katika uwanja wa Mkendo mjini Musoma mkoa wa Mara leo Jumamosi Septemba 5, 2020
Mama Janeth Magufuli akizungumza jambo na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere alipojiunga na wananchi wa mkoa wa Mara kumsikilizaMgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala Rais Dkt John Pombe Magufuli katika mkutano wa hadhara wa kampeni katika uwanja wa Mkendo mjini Musoma mkoa wa Mara leo Jumamosi Septemba 5, 2020
Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere akisalimiana na Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala Rais Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni katika uwanja wa Mkendo mjini Musoma mkoa wa Mara leo Jumamosi Septemba 5, 2020
No comments:
Post a Comment