Bondia Mtanzania kutoka Mji kasoro Bahari Cosmas Cheka ameibuka mshindi wa Mchezo wa Masumbwi baada ya kumchapa mpinzani wake kutoka Malawi Hannock Phiri na kufanikiwa kuchukua Mkanda wa wa Ubingwa wa UBO.
Cheka ameshinda kwa point baada ya kufanikiwa kumaliza 'round' 12 za mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhiri usiku wa Septemba 13,2029 na kushuhudiwa na mamia ya watazamaji.
Wadau mbalimbali wa mchezo huo wamesema kuwa Mchezo huo umeanza kurudisha hesima yake na umaarufu wake baada ya wadau wa mchezo huo kujitokeza na kudhamiria kuurudisha mchezo wa ngumi kwenye hadhi hadhi yake huku wakiipongeza kituo Cha habari cha Azam Tv kutoa udhamini wa kuonyesha Michezo mbalimbali ukiwemo mchezo wa Masumbwi.
No comments:
Post a Comment