Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
ILANI ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 imetaja mambo yatakayozingatiwa katika kutekeleza vipaumbele vikuu vya Ilani hiyo kwa ajili ya kuleta maendeleo ya Watanzania.
Kupitia muhutasari wa Ilani hiyo ambayo imeelezwa kwa kina wakati wa uzinduzi wa Kampeni za mgombea urais wa Chama hicho Dk. John Magufuli imesema kuwa itaendelea kulinda na kuimarisha utu, usawa, haki na uongozi bora ili kudumisha amani, umoja na mshikamano wa Taifa letu.
Chama hicho kimesema kitaendelea kudumisha na kuimarisha umoja,udugu, mshikamano, amani, utulivu, ulinzi na usalama.Pia kuendelea kuimarisha Muungano wa serikali mbili, kuenzi Uhuru wa nchi yetu na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar pamoja na kutumia tunu nyingine za kitaifa ikiwemo falsafa ya Mwenge wa Uhuru katikakujenga moyo wa uzalendo wa kitaifa na uwajibikaji.
CCM kupitia mgombea wake urais Dk.John Magufuli kimefafanua kwa kina kuhusu Ilani hiyo ambapo mambo mengine yatakayoendelezwa ni kuendelea kuimarisha demokrasia, utawa la bora na haki za binadamu na mapambano dhidi ya rushwana ufisadi, pamoja na udhalilishaji wa aina zote.
Pia kuendelea kuimarisha Serikali za Mitaa ili ziweze kutimiza wajibu wao kwa wananchi katika maeneo husika, kuendelea kujenga mazingira wezeshi kwa asasi za kiraia, kidini na vyombo vya habari kustawi ili kuchangia katika maendeleo yaTaifa na kuendelea kuimarisha huduma na kulinda haki kwamakundi maalum wakiwemo wanawake, vijana,wazee, watoto na watu wenye ulemavu.
Mengine ni kukuza uchumi wa kisasa, fungamanishi, jumuishina shindani uliojengwa katika msingi wa viwanda, huduma za kiuchumi na miundombinu wezeshi, kuendelea kujenga na kukuza uchumi shindani hususan kupitia sekta za viwanda na huduma za kiuchumi utakaowezesha ustawi wa wananchi wote.
CCM kupitia mgombea wake Dk.Magufuli imesisistiza kuendelea kuimarisha miundombinu ya kimkakati ili kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi kufanya shughuli zao kwa ufanisi na tija,kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kukua na kustawi pamoja na kuvutia wawekezaji ili watoe mchango stahiki katika maendeleo ya nchi yetu.
Pia kuendelea kuboresha masilahi na mazingiraya kazi kwa wafanyakazi katika sekta zote,kuongeza faida ambazo nchi yetu inapata kutokana na maliasili zetu na utajiri wa nchi kwa kuimarisha usimamizi wa mikataba ya uzalishaji na kujenga uwezo wa ndani wa kuvuna na kuchakata rasilimali hizo na kuimarisha usimamizi na uhifadhi wa mazingira na uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Chama hicho kupitia Ilani hiyo ambayo imeelezwa kwa kwa kina na Dk.Magufuli ni kwamba itatenga maeneo maalum ya akiba ya ardhi na uwekezaji,kuendelea kuimarisha mawasiliano ya simu za mkononi nchini ili yaweze kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa maendeleo ya wananchi.
Kuendeleza diplomasia ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni ikiwa ni pamoja na kufanya lugha ya Kiswahili kutumika kikamilifu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC),Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC), Umoja wa Afrika(AU) na Umoja wa Mataifa(UN).
Pia kuleta mageuzi ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kuwa na uhakikawa chakula na kujitegemea kwa chakula wakati wote na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya uchumi, kuhakikisha uzalishaji unaongezeka katika mazao ya chakula,ufugaji na uvuvi kwa ajili ya kujitosheleza kwa chakula na lishe bora.
Kupitia Ilani hiyo ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020, CCM imeeleza kuongeza tija katika kilimo, ufugaji na uvuvi kwa ajiliya kuchochea maendeleo ya uchumi hasa katika sekta za viwanda na huduma, kuimarisha ushirika ili kuunganisha nguvu za wazalishaji hasa katika kupata pembejeo na kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi.
Pia kuimarisha miundombinu na kuongeza maeneo ya umwagiliaji katika kilimo ili kupata mazao mengi zaidi kwa wakati wote wa mwaka na kukamilisha na kutekeleza mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya shughuli za kijamii, uwekezaji na uzalishaji na kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za Afya, Elimu,Maji,Umemena Makazi vijijini na mijini.
Katika muhutasari huo wa Ilani CCM kupitia Mwenyekiti wake Dk.Magufuli umeeleza kuwa wataongeza kasi ya usambazaji maji safi na salama ili kutosheleza mahitaji kwa zaidi ya asilimia 85 vijijini na zaidi ya asilimia 95 kwa mijini kwa upande wa Tanzania Bara ifikapo mwaka 2025 na zaidi ya asilimia 95 kwa upande wa Zanzibar.
Pia kuendelea kuimarisha mfumo wa elimu ili uweze kuzalisha wataalam mahiri zaidi wenye uwezo katika sayansi,teknolojia,ufundi na nyanja nyingine ambao wanaweza kujiajiri na kuajirika ndani ya nchi na mahali popote duniani, kusambaza umeme kwenye mitaa na vijiji vyote ifikapo mwaka 2025;
Mengine yatakayoendelezwa na CCM ni kutoa huduma za afya kwa wote, kuhamasisha na kuweka mazingira wezeshi ili wananchi katika maeneo yote nchini wawe na makazi bora, kuchochea matumizi ya utafiti, sayansi, teknolojia na ubunifu kama nyenzo ya maendeleo ya haraka ya kijamii na kiuchumi na kuimarisha na kuhuisha taasisiza utafiti, sayansi, teknolojia na ufundi ili ziweze kubuni nyenzo za kuongeza tija katika sekta za uzalishaji na huduma;
CCM kupitia Ilani hiyo ya uchaguzi imesisitiza kwamba itahakikisha kila shule ya sekondari nchini ina kuwa na kompyuta na huduma za intaneti,kusomesha Watanzania nje ya nchi katika vyuo bora na maalum dunia ni kwenye masuala ya sayansi,tiba, teknolojia na maeneo mengine yenye umuhimu ili kupata maarifa bora na ya kisasa na ujuzi ili kuchochea maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini na kuchochea na kuendeleza ubunifu,uvumbuzi na ugunduzi nchini kwa ajili ya maendeleo yaTaifa.
Mengine yakayotekelezwa ni kutengeneza ajira zisizopungua milioni nane katika sekta rasmi na isiyorasmi kwa ajili ya vijana,kuchochea ukuaji wa uchumi hususan katika sekta ya viwanda vinavyotumia malighafi za kilimo, mifugo,uvuvi,madini,maliasili na sektaya huduma za kiuchumi ikiwa ni pamoja na utalii.
Pia kuwawezesha vijana kushiriki katika shughuli za ujasiriamali, ikiwemo kuwapatia mafunzo na kuwaunganisha na taasisi na asasi za utoaji mikopo yenye riba na masharti na fuu, kuwahamasisha na kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika utamaduni, michezo na sanaa kwa ajili ya afya bora na burudani na pia kuongeza fursa za ajira na kipato na kuhakikisha kuwa miradi mikubwa ya kimkakati inaajiri vijana wengi zaidi wa Kitanzania.
No comments:
Post a Comment