Na Yassir Simba,Michuzi Tv
Safari ya kuuanza msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara imeanza leo 30 mwezi Agosti 2020 katika dimba Benjamin Mkapa kwa Yanga kutambulisha wachezaji wapya pamoja na benchi la ufundi katika kilele cha wiki ya mwananchi.
Sherehe hizo za kilele cha wiki ya mwananchi ziliambatana na utambulisho wa baadhi nyota wapya waliosajiliwa na klabu hiyo wakiwemo Tuisila Kisinda,Mukoko Tonombe,Michael Sarpong,Shomary Kibwana, Bakari Mwamnyeto,Zawadi Mauya,Waziri Junior pamoja na Carlos Carlinhos.
Katika kilele cha wiki ya Mwanachi klabu ya Yanga ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Aingle Noir kutoka nchini Burundi ambapo mtanange huo ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2 -0.
Mabao ya Tuisila Kisindi katika dakika ya 39 na bao la Michael Sarpong katika ya 52 ya mchezo yalitosha kuwafanya mashabiki wa Yanga kutembea kifua mbele kwamba wanasilaha nzito sana katika kikosi chao.
Pia katika mchezo huo iliwalazimu wageni wa mchezo huo timu ya Aingle Noir kucheza pungufu kutokana na na kadi nyekundu aliyoadhibiwa mchezaji wa timu hiyo Koffi Kouassi katika dakika 29 ya mchezo mara baada ya kupata kadi mbili za njano ambazo zilizaa kadi nyekundu.
Hata hivyo kilele hicho cha wiki ya mwananchi kilinogeshwa na burudani mbalimbali zikiwemo maonyesho tofauti kutoka kwa wasanii wa bongofleva akiwemo Baba Levo, TMK Family, Chege,Shilole,Mzee Wa Bwax pamoja na Msanii Harmonize kutoka label ya muziki ya kondeang ambaye alifanya onyesho la aina yake huku akiingia uwanjani kwa staili ya kijeshi kwa kutumia kamba kutoka angani huku akiiakata kiu ya burudani ya maelfu ya mashabiki waliofika uwanja wa Mkapa jijini Dar Es Salaam.
Hadi dakika 90 za mchezo zinaisha Yanga wanaibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Warundi klabu ya Aingle Noir
No comments:
Post a Comment