Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Kimanta amepokea treni ya kwanza ya abiria kutoka Moshi mkoani Kilimanjaro na mizigo kutoka Tanga ikiwa na tani 320 za saruji kutoka Kampuni ya Tanga Cement.
Mkuu wa mkoa amepokea treni hiyo jana Agosti 24,2020 saa 9:30 alasiri kwenye stesheni ya Krokon jijini Arusha na na kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwira, kisha akapanda kwenye treni hiyo saa 9:35.Akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Arusha na wengine kutoka mikoa jirani, Mkuu wa mkoa alisema amefurahi kupokea treni hiyo yenye mabehewa nane ya abiria na treni ya mzigo yenye mabehewa nane ya saruji yenye uzito wa tani 320 kutoka Kampuni ya Saruji ya Tanga.
Alisema kukamilika kwa kipande cha reli ya Moshi - Arusha na kuanza kutoa huduma, ni mwendelezo wa utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji inatoa fursa za kibiashara.
Hatutamvumilia mtu yeyote atakayehujumu miundombinu ya reli,î alisema Mkuu wa mkoa huyo.
Mkuu wa mkoa amewataka viongozi na watendaji wa mikoa na maeneo ambayo reli inapita kuhakikisha wanatunza miundombinu na kutoa elimu kwa umma kuhusu usalama.
Katika treni hilo la abiria, alikuweno Mgwira na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hamphrey Polepole na viongozi wengine wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Akitoa taarifa kuhusu mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alisema gharama za kufufua reli ni sh. bilioni 14, fedha ambazo ni kodi ya wananchi.
Alisema treni ya abiria ilisitishwa tangu mwaka 1994, wakati ya mizigo ilikuwa haifanyi kazi kwa miaka 12, lakini huduma hizo sasa zinarejea.
Kadogosa alisema kuwa, watajenga treni ya kisasa kutoka Tanga-Arusha hadi Musoma mkoani Mara, ikiwa ni jitihada za Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli.
Wenzetu wa Tanga Cement (TCPLC), ujio wa reli hii, liangalieni suala la bei ya saruji, ikiwezekana ipungue kama nasi tulivyofanya kwenu alisema Kadogosa.
Amesema nauli kutoka Arusha hadi Dar es Salaam wamependekeza kuwa shilingi 18,000/=
No comments:
Post a Comment