Wachezaji wa timu ya Simba wakiwa katika picha ya pamoja na Ngao Jamii baada ya kuitwaa jioni ya leo katika Dimba la Sheikh Amri Adeid, jijini Arusha.
Charles James, Michuzi TV
MABINGWA wa Soka nchini Klabu ya Simba leo imefanikiwa kushinda mchezo wake wa Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo FC ya Mkoani Mtwara katika mchezo uliopigwa jioni ya leo jijini Arusha.
Mchezo huo wa Ngao ya Jamii uliwakutanisha Mabingwa wa Ligi Kuu ambao ni Simba na Namungo FC ambayo ilishika nafasi ya pili kwenye Michuano ya Shirikisho maarufu FA.
Staa wa Timu hiyo raia wa Ghana, Benard Morrison aliichezea Simba mchezo wake wa kwanza wa mashindano baada ya sakata lake la usajili kutokea Yanga ambapo aliifungia timu yake mpya bao la pili huku akisababisha penati iliyofungwa na Nahodha, John Bocco.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Van De Broeck amekipongeza kikosi chake kwa ushindi huo ambao umewafanya kutwaa taji la kwanza huku akiahidi kufanya vizuri zaidi kwenye Michezo ya Ligi Kuu.
No comments:
Post a Comment