Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna. |
Mwenyekiti wa Bodi ya NMB, Dk. Edwin Mhede alimtangaza Zaipuna huku akikiri kuwa mchakato wa kumpata haukuwa mwepesi lakini hakukuwa na upendeleo isipokuwa walitazama wasifu, utendaji na maslahi ya Benki na Tanzania.
Dk. Mhede alisema katika kipindi kirefu Benki hiyo ilikosa mtu baada ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wake kuondoka na hivyo walibaki na mtu aliyekuwa anakaimu kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu lakini takwa la kisheria lilikuwa linawabana kuwa ni lazima wapate mtu.
Zaipuna anakuwa Mtanzania wa kwanza kushika nafasi hiyo tangu Benki hiyo ilipobinafsishwa ambapo kwa nyakati zote nafasi za juu zilishikwa na wageni wakiwemo Ineke Bussemaker aliyekuwa Mkurugenzi tangu 2014 – 2018 kisha nafasi hiyo ikachukuliwa na Albert Jonkergow ambaye alishikiria kwa kipindi cha mpito cha miezi sita kabla ya Zaipuna kupewa nafasi ya kukaimu.
Mwenyekiti alisema mchakato wa kumpata Mtendaji Mkuu ulikamilika Juni 30,2020 na jana ilikuwa ni siku ya kumtangaza huku akibainisha kuwa sifa zote zilizotakiwa katika nafasi hiyo, walijiridhisha kuwa Zaipuna anazo hivyo hakuna shaka kuhusu utumishi wake katika nafasi hiyo.
"Katika kipindi chote tulihangaika kumpata mtu mwenye kufikia vigezo vinavyotakiwa, lakini wakati mwanamama huyu alipokuwa anakaimu, Benki imeendelea kufanya vizuri zaidi na kukuza mtaji wake, hakuna mahali paliyumba chini ya usimamizi wake,hivi kwa hali hiyo mnadhani tungefanyaje," alisema Dk. Mhede.
No comments:
Post a Comment