A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, August 17, 2020

MWANGA HAKIKA MICROFINANCE BANK, BENKI MPYA BAADA YA KUUNGANA KWA BENKI TATU (MWNAGA BANK, HAKIKA NA EFC BANK)

 

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Dk. Bernard Kibesse (kushoto), Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya (katikati) wakifuatilia zoezi la uzinduzi wa benki ya Mwanga Hakika Microfinance Ltd. Benki hiyo ni muunganiko wa benki tatu (Mwanga Community bank, Hakika Microfinance Bank na EFC Tanzania Microfinance Bank). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Mwanga Hakika Microfinance Ltd.
Naibu Gavana wa BOT, Dk. Bernard Kibesse (kulia), Naibu Mwekezaji, Raymond Tarimo pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Mhandishi Ridhuan Mringo wakifurahi baada ya kuzindua benki mpya iitwayo Mwanga Hakika Microfiance Bank baada ya muunganiko wa benki tatu tatu (Mwanga Community bank, Hakika Microfinance Bank na EFC Tanzania Microfinance Bank).Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Jagjit Singh.
Naibu Gavana wa BOT, Dk.Bernard Kibesse akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi benki ya Mwanga Hakika Microfinance Bank iliyotokana na muunganiko wa benki tatu ikiwamo Mwanga community Bank, Hakika Microfinance Bank Pamoja na EFC Tanzania Microfinance Bank. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi, Eng. Ridhuan Mringo.

Dk. Gabriel Ndunga, mteja wa kwanza kupata huduma kutoka benki mpya ya Mwanga Hakika Microfinance Bank iliyozinduliwa jana baada ya kuungana kwa benki tatu ikiwamo Mwanga Community Bank, Hakika Microfinance Bank Pamoja na EFC Tanzania Microfinance Bank.
  • Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza uimara wa benki katika utoaji wa huduma pamoja na ubunifu.
Dar es Salaam. Agosti 14, 2020. Mwanga Community Bank Ltd, Hakika Microfinance bank Ltd na EFC Tanzania Microfinance zimefanikiwa kuungana na kuwa benki moja ijulikanayo kama ‘Mwanga Hakika Microfiance Bank Ltd’, hatua inayoashiria ukuaji wa sekta ya kibenki nchini.

Muunganiko huo umefanikiwa kufuatia uthibitisho kutoka benki ya Tanzania (BoT) pamoja na Tume ya ushindani (FCC) na kupelekea kuundwa kwa Benki moja yenye thamani ya 40.5 bilioni ya mali.Pia, benki hiyo inatarajia kuongeza nguvu ya ushindani katika soko nchini.

Muungano huo ulizinduliwa rasmi katika hafla iliyohudhuriwa na Naibu Gavana wa BoT, Dk.Bernard Kibesse na kushuhudiwa na wadau mbalimbali kutoka sekta ya fedha.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages