KATIBU Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila anatarajia kukutana na watendaji wa Tume ya Madini jijini Arusha kwa lengo la kujadili mafanikio ya Tume ya Madini kwa Mwaka wa Fedha 2019-2020, changamoto na mikakati ya namna bora ya utekelezaji wa mpango kazi wa Tume kwa mwaka wa fedha 2020-2021.
Jana Julai 23,2020 kunafanyika kikao cha awali kitakachoshirikisha mameneja kutoka Tume ya Madini Makao Makuu na Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa Nchini.
Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Arusha, Hamis Kamando akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Maafisa madini wakazi wa nkoa wakifuatilia mkutano
Meneja rasilimaliwatu, Gift Kilimwomeshi akizungumza kwenye kikao hicho kilichowashirikisha mameneja kutoka makao makuu tume ya madini
No comments:
Post a Comment