Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MSANII wa muziki wa kizazi kimya nchini Benard Paul ‘Ben Pol’ amekuwa ni miongoni mwa wasanii 10 wa Afrika walioimba wimbo maalum wa kujilinda na maambuzi ya ugonjwa wa Corona wa Stand Together.
Akizungumza na michuzi Blog, Ben Pol amesema kuwa wimbo huo unaitwa Stand Together, ambao umeshirikisha wasanii 2face Idibia kutoka nchini Nigeria, Ahmed Soultan wa Morocco, Teni, Yemi Alade wote kutoka Nigeria na Amanda Black kutoka Afrika Kusini.
Amesema, wasanii wengine ni Stanley Enow wa nchini Cameroon, Gigi LaMayane wa Afrika Kusini, Prodigio kutoka nchini Angola na Betty G wa Ethiopia.
Ben Pol ameeleza kuwa lengo ni kuhamasisha Afrika nzima kuendelea kuchukua taadhari ya kujinga na maambuziki ya ugonjwa huo ambao umekuwa tishio katika kila nchini.
"kuna baadhi ya nchini za Afrika zina ukaribu wa kuingia nchi moja baada ya nyingine hata baadhi ya familia kujumuika pamoja, ambapo sasa imekuwa tofauti, ambapo kila mmoja anahitajika kumuelemisha mwingine ili ugonjwa huo uondoke Afrika na dunia kwa ujumla," amesema
“Tumefanya wimbo huu lengo ni kuhamasisha Afrika nzima, kuendelea kuchukua taadhari , kila mmoja wetu aendelee kuhamasisha ikiwa ni pamoja na kujilinda na kuwalinda wengine, wajiepushe na Corona,"
Aidha Ben Pol amewataka wananchi kuendelea kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo ambapo kuna baadhi ya nchini barani Afrika bado wana tatizo kubwa na wananchi wake kupatwa na maambuziki ya ugonjjwa huo.
No comments:
Post a Comment