Benki ya NMB imetoa msaada wenye thamani ya shilingi Milioni 36 kwa shule Saba za Sekondari; Kirare, Japan, Chongoleani, Nguvumali, Pongwe na Galanos za Jijini Tanga, kwa kuzipatia madawati 250 pamoja na mabati 352 ili kutatua changamoto za kielimu.
Akikabidhi msaada huo katika Shule ya Sekondari ya Pongwe kwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki hiyo, Benedicto Baragomwa alisema, wamekuwa mstari wa mbele kushiriki kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.
Alisema kwa upande wa sekta ya elimu, kipaumbele wamekiweka kwenye madawati, vifaa vya kuezekea huku kwenye afya wakitoa vifaa vya tiba kama vitanda vya kujifungulia wakina mama na vitanda vya wagonjwa na magodoro yake vilevile na kusaidia majanga yanayoipata nchi.

No comments:
Post a Comment