A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, June 10, 2020

WAZIRI JAFO ARIDHISHWA NA KASI UJENZI WA HOSPITALI YA UHURU, ATOA MAAGIZO KWA TBA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa Wakala wa Majengo Nchini (TBA) alipofika kutembelea ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa wilayani Chamwino, Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo (kulia) akikagua ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa wilayani Chamwino, Dodoma. Ziara hiyo ameifanya leo ambapo aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge (katikati).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo akipokea maelekezo kutoka kwa Mhandisi wa Ujenzi wa Hospitali ya Uhuru kutoka Suma JKT, Mhandisi Omari Kabaluga wakati alipofika kukagua maendeleo ya ujenzi huo leo wilayani Chamwino, Dodoma.

Charles James, Michuzi TV
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo ameuagiza Wakala wa Majengo  (TBA) kukaa na Wahandisi wanaojenga Hospitali ya Uhuru Chamwino, Dodoma ambao ni Suma JKT ili kujua kama wataongeza ghorofa ya pili kwenye Hospitali hiyo.

Maagizo hayo ameyatoa leo wilayani Chamwino alipoenda kutembelea ujenzi wa Hospitali hiyo ambayo kwa mujibu wa Mhandisi wa Suma JKT, Omari Kabalagu inatarajia kukamilika Agosti mwaka huu.

Akizungumza baada ya kumaliza kukagua ujenzi huo, Waziri Jafo amepongeza kasi yake ambapo amesema kukamilika kwa hospitali hiyo kutaifanya iwe miongoni mwa hospitali nzuri na za kisasa nchini.

Jafo amesema ameshuhudia mabadiliko makubwa ya ujenzi huo kulinganisha na alipofika hapo mara ya mwisho na kuongeza kasi na uzalendo wa kufanya kazi kwa weledi unaooneshwa na Suma JKT.

" Niwapongeze sana ndugu zangu wa Suma mnafanya miradi mingi sana nchini na hakika kila mmoja ameshuhudia kasi kubwa na ubora wa kazi ambao mmeuonesha.

Sasa niwatake TBA kuhakikisha hadi kufikia Jumatatu mnakuja na majibu ya uhakika ya kitaalamu kama uwezekano wa kuongeza floo ya pili upo au vipi, tunataka Hospitali hii ikikamilila iendane na hadhi ya jina lake la Uhuru," Amesema Jafo.

Waziri Jafo pia amepongeza utendaji kazi wa Mhandisi wa ujenzi huo, Omari Kabalagu akisema ameonesha ukomavu na weledi wa hali ya juu tangu kuanza kwa ujenzi was hospitali hiyo.

" Kwenye sifa lazima tutoe sifa, Suma JKT mmefanya kazi kubwa sana na huyu mhandisi wenu ameonesha uwezo mkubwa, ni kijana mdogo lake mwenye uwezo kama jambo haiwezekani anakuambia kama haliwezekani lakini tutafanya hivi na hivi, nampongeza sana," Amesema Jafo.

Hospitali ya Uhuru wilayani Chamwino inajengwa baada ya Rais Magufuli kuelekeza kufanya hivyo katika sherehe za Uhuru mwaka 2018 na kuelekeza fedha zilizokua zitumike kwenye maadhimisho ya sherehe hizo kujenga Hospitali hiyo mkoani Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages