Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Stephen Mhapa akiwa anatekeleza majukumu yake akiwa kwenye baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Iringa ( PICHA KUTOKA MAKTABA)
Diwani wa kata ya Maboga Veny Muyinga akiongea waandiahi wa habari kuhusiana na maendeleo y kata hivyo.
(PICHA KUTOKA MAKTABA)
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Stephen Mhapa akifurahia jambo na wananchi wa jimbo la kalenga
Na Fredy Mgunda, Iringa
WANANCHI wa jimbo la kalenga mkoani Iringa wamewataka diwani wa kata ya Maboga Veny Muyinga na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa na diwani wa kata ya Nzihi Stephen Mhapa kugombea ubunge katika jimbo hilo kutokana na kazi kubwa za kimaendeleo walizozifanya.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi walisema kuwa wapo tayari kuwachukulia fomu za kuwania nafasi ya ubunge kwenye ngazi ya chama kwa kuwa wanaimani na madiwani hao.
Wakimzungumzia mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Stephen Mhapa walisema kuwa anafanya kazi kubwa kama mbunge wa jimbo la kalenga wakati yeye ni mwenyekiti wa halmashauri tu.
Walisema kuwa kazi za kimaendeleo katika jimbo la kalenga zimefanywa na mwenyekiti Mhapa zaidi kuliko viongozi wengi kwa kuwa aligundua na kujua shida za wananchi wa jimbo hilo.
"Sisi wananchi wa jimbo la kalenga tulikuwa kama yatima kimaendeleo lakini mwenyekiti Mhapa alikuwa ndio anatufaliji kwa kutupambania katika kuleta maendeleo hivyo sasa ni muda wake wa kuwa mbunge wa jimbo la kalenga"walisema
Walisema kuwa ukipita kila kata utakutana na kazi kubwa ya kimaendeleo iliyofanywa na mwenyekiti Mhapa hivyo ndio sababu ya kusema kuwa wananchi wapo tayari kumchukulia fomu za kugombea kwa kuwa anauwezo huo.
Baadhi ya wananchi hao walisema kuwa wapo tayari kwenda kumchukulia fomu za kugombea kwenye kura za maoni za chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuwa bado ndio mwanachama wa chama hicho.
Kwa upande mwingine baadhi ya wananchi walisema diwani wa kata ya Maboga Veny Muyinga walisema kuwa amekuwa anafanya maendeleo makubwa kwenye kata yake na amekuwa na falsafa za kibunge.
Walisema kuwa diwani huyo alipitia kipindi kigumu mara baada ya kupata ajali lakini akiwa anaumwa aliendelea kujitolea kufanya shughuli za kimaendeleo huku akiwa bado anaumwa.
"Ukienda kwenye kata ya Maboga ukamsema vibaya diwani huyo unaweza kupigwa na wananchi wa kata hiyo kutokana na kazi kubwa za kimaendeleo ambazo zimefanywa na diwani ndio maana tumasema kuwa anafaa na sifa za kugombea jimbo la kalenga"walisema wananchi
Walisema kuwa diwani Veny Muyinga alipambana sana kuhakikisha hospitali ya wilaya inajengwa katika jimbo la kalenga jambo mambo haya kwenda sawa juhudi zake yeye na mwenyekiti Mhapa zilionekana na sababu kubwa hawa wawili mmoja wapo anastahili kuwa mbunge wa jimbo la kalenga
No comments:
Post a Comment