A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, June 15, 2020

DK KALEMANI ATOA ONYO KWA WAFANYABIASHARA WATAKAOPANDISHA BEI YA MAFUTA

 Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani akizungumza na watendaji wa Wizara yake na Wandishi wa habari leo jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo kuhusiana na bei ya mafuta ambapo amewataka wafanyabiashara kufuata bei elekezi iliyopangwa na Serikali.

Charles James, Michuzi TV
SERIKALI imetoa onyo kali kwa wafanyabiashara wa mafuta watakaokaidi maagizo yake kwa kuuza mafuta kwa bei kubwa tofauti na bei elekezi iliyopangwa.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani leo amewataka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kufanya uchunguzi wa siku saba kuwabaini wale wote wanaokwenda kinyume na maelekezo ya serikali.

Dk Kalemani amewataka EWURA kufanya ufuatiliaji huo na ndani ya muda aliowapatia wamletee majibu ya kina ya akina nani ambao wamekaidi agizo la serikali ili waweze kuchukuliwa hatua.

Waziri Kalemani amewataka wafanyabiashara wa mafuta kutambua ya licha ya kwamba wanafanya biashara ambayo pia inaingizia serikali kodi lakini pia wanatoa huduma hivyo haiwezekani kutoa huduma inayowaumiza wananchi.

Ametoa onyo pia kwa wafanyabiashara ambao kipindi hiki ambapo mafuta yameshuka bei wao wanatumia mwanya huo kuyaficha ili waje kuyauza kipindi ambacho yatakua yamepanda bei.

" Zipo taarifa za baadhi ya maeneo kuwepo kwa wafanyabiashara ambao wanaficha mafuta tu kwa sababu yameshuka bei ili waje kuuza pindi bei itakapopanda nitoe onyo kwao wasijaribu kufanya huo uhujumu.

Lakini pia kwa wale watakaouza bei tofauti na iliyopangwa watambue sheria ya EWURA iko wazi kabisa kwamba faini yake ni Sh Milioni 100 au kusitishwa kwa shughuli zao," Amesema Dk Kalemani.

Waziri Kalemani amesema ndani ya miezi sita ijayo wanategemea kuanzisha mradi nafuu wa kupeleka mafuta Vijijini ili kutoa unafuu kwa wananchi kuweza kupata mafuta kwa urahisi.

" Tunategemea ndani ya miezi sita tuwe na vituo vidogovidogo vya mafuta na huduma tembezi (mobile) na hasa vipaumbele kwenye maeneo yenye changamoto ya miundombinu ya barabara na ya visiwani.

Lengo letu ni kuepusha gharama za ununuzi wa mafuta kwa wananchi wetu lakini pia kuepusha hatari inayoweza kutokea kwa wananchi wanaobeba mafuta kwenye vidumu na chupa," Amesema Waziri Kalemani.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages