Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ametangaza rasmi kuanzia tarehe 29, Juni, 2020 Shule Zote zifunguliwe ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kwa shughuli mbalimbali za kijamii ili maisha yaendelee kutokana na kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa wa Corona nchini.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo juni 16 alipokuwa akilihutubia na kulifunga Bunge la 11 jijini Dodoma ambapo amesema kuwa kwa sasa maambukizi ya Corona yamepungua kwa kiasi kikubwa na hivyo umefika wakati wa kufungua shughuli zote zilizokuwa zimesimama ikiwemo kufunguliwa kwa Shule.
“Kutokana na mwendendo wa corona kuendelea kuwa mzuri, corona imepungua sana, naomba nitangaze kuanzia June 29 mwaka huu nafikiri itakuwa Jumatatu, shule zote zilizokuwa zimebaki zifunguliwe, lakini Watanzania waendelee kuchukua tahadhari”-JPM.
No comments:
Post a Comment