Mawe makubwa mawili ya Tanzanite moja lina kilo 9.2 ambalo lina thamani ya shilingi bilioni 4.5 na la pili lina kilo 5.8 lenye thamani shilingi bilioni 3.3.
Afisa Madini akionyesha moja ya jiwe la Tanzanite lilipatikana
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila amesema kuwa leo Wizara inamtabua Mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite Bw. Saninniu Laizer kuwa bilionea baada ya kupata mawe makubwa mawili yenye thamani ya shilingi bilioni 7.8.
Katibu Mkuu amesema kuwa mchimbaji huyo amepata mawe hayo mawili ambapo moja lina kilo 9.2 ambalo lina thamani ya shilingi bilioni 4.5 na la pili lina kilo 5.8 lenye thamani shilingi bilioni 3.3.
Mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite Bw. Saniniu Laizer bilionea mpya Tanzania
“Na utofauti wake ni kwamba mawe ya uzito huo hayajawahi kupatikana kwenye machimbo ya tanzanite tangu machimbo yaanze na yamepatikana ndani ya ukuta wa Mirereni kwahiyo hii ni rekodi mpya ya kupata mawe yenye uzito huo” amesema Prof. Msanjila
Profesa Msanjila amesema kuwa sekta ya madini inauwezo wa kumfanya mtu kuwa bilionea kwa haraka, ameongeza kuwa kunahitaji kuwa uwekezaji wa dhati katika sekta hiyo.
No comments:
Post a Comment