A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, May 9, 2020

Watanzania miongoni mwa visa vipya vya corona Kenya

Idadi ya maambukizi ya virusi vya corona nchini Kenya imepanda hadi kufikia jumla ya watu 649 Jumamosi, baada ya kutangazwa kwa matokeo chanya vya virusi katika sampuli za watu 28 miongoni mwa waliopimwa.

katibu wa kudumu katika wizara ya afya nchini humo Rashid Aman amesema kuwa 24 miongoni mwa wagonjwa hao wapya ni raia wa Kenya, wanne miongoni mwao wakiwa ni Watanzania.

Bwana Aman ameongeza kusema kuwa idadi ya waliopona wameongezeka na kufikia hadi 207, huku wagonjwa wengine watano zaidi wakiruhusiwa kwenda nyumbani .

Idadi ya vifo kwa sasa imepanda hadi watu 30.

Amesema kuwa mgonjwa mmoja zaidi amefariki dunia katika kaunti ya Mombasa.

Wakati hayo yakijiri katika kaunti ya Mombasa Ijumaa, polisi walitangaza kuwa mmoja wa watu watano waliotoroka kutka nyumbani kwao baada ya kupatikana na virusi amepatikana akiwa amekufa.

Katibu huyo wa kudumu wa Wizara ya Afya amesema kuwa wagonjwa hao wapya wa Covid-19 ni miongoni mwa watu 1,611 waliopimwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita na kwamba hadi kufikia Me, 9, Kenya imekwishapima jumla ya sampuli 31,041 .

Amesam watu10 walipatikana kutoka Mombasa, tisa Nairobi, wanne Migori, wawili Kajiado na wengine mmoja mmoja kutoka kaunti zaq Machakos, Kiambu na Homa Bay.

Huku idadi ya visa vya maambukizi ya corona vikiendelea kupanda kwa siku chache zilizopita, wizara ya Afya ya Kenya imeuonya umma dhdi iya kurejea katika maisha ya kawaida, akisema kuwa bado Kenya haijashinda mapambano dhidi ya ugonjwa hatari.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages