A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, March 2, 2020

Virusi vya Corona: Idadi ya vifo yafikia elfu 3 kote duniani


Idadi ya waliofariki kutokana na janga la virusi vipya vya Corona kote ulimenguni imepita watu elfu 3 hii leo baada ya wengine wengi kufariki katika kitovu cha mripuko huo nchini China na visa kuongezeka kote ulimwenguni huku Marekani ikirekodi kifo cha pili.

Kufikia sasa, virusi hivyo vimewaathiri zaidi ya watu elfu 89 na kusambaa katika zaidi ya mataifa 60 baada ya kuzuka kwa mara ya kwanza nchini China mwishoni mwa mwaka jana.



Korea Kusini iliyo na idadi kubwa zaidi ya maambukizi nje ya China, imeripoti takriban visa 500 vipya hii leo na kufikisha idadi yake ya maambukizi kuwa zaidi ya elfu 4.

Takriban nusu ya visa vya maambukizi nchini Korea Kusini vinahusishwa na kundi moja la kidini ambalo kiongozi wake aliomba radhi hii leo kwa kusambaa kwa virusi hivyo.

Serikali ya Korea Kusini imewataka waendeshaji mashtaka nchini humo kufungua mashtaka ya mauaji dhidi yake.

Wakati hofu ikiongezeka kuhusu kuenea kwa janga hilo, shirika la afya duniani WHO limezihimiza nchi zote kuweka tayari vifaa muhimu vya kujikinga wakati wa kupumua kuwatibu wagonjwa walio na dalili mbaya za ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages