A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, March 2, 2020

Nchimbi atuma salamu Mbao FC


Mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi, amesema kuwa akipata nafasi kesho mbele ya Mbao atapambana kuipa ushindi timu yake kwa kushirikiana na wachezaji wenzake.

Ndani ya Ligi Kuu Bara, juzi Uwanja wa Taifa alifunga mabao mawili yaliyoipa pointi tatu timu yake ya Yanga mbele ya Alliance.



Nchimbi amesema, "Kazi ni nzito kwenye ligi na mashindano ambayo tunashiriki, ninachokifanya ni kuona ninakuwa bega kwa bega na wachezaji wenzangu ili kuona namna gani tunapata matokeo hata mchezo wetu wa kesho dhidi ya Mbao tutapambana kupata matokeo," .

Kesho Yanga itashuka Uwanja wa Taifa kumenyana na Mba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa majira ya saa 1:00 usiku.a

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages