Mwanamuziki Nassibu Abdul 'Diamond Plutnumz' amepelekwa mahakamani kwa tuhuma za uharibifu wa mali ndani ya nyumba aliyokuwa amepanga kwa ajili ya studio maeneo ya Sinza Kijitonyama kabla ya kuhamia Mbezi, jijini Dar es Salaam huku akidaiwa kodi ya mwaka mmoja.
Mali hizo zenye thamani ya zaidi ya Sh337 milioni kwa mujibu wa wasanifu majengo waliofanya uchunguzi wa vitu vilivyoharibika vya Maulidi Wandwe ambazo Diamond Plutnumz anatakiwa kulipa.
Diamond amepelekwa Mahakama ya Ardhi Mwananyamala Dar es Salaam leo Jumatatu na mmiliki wa nyumba hiyo Maulid Wandwi ambapo msanii huyo hakutokea mahamani huku wakili wake Gerald Hamisi alitoa taarifa kwamba mteja wake yupo nje ya nchi hivyo kutokana na ugonjwa wa Corona hatarudi nchini baada ya wiki tatu.
Aidha wakili huyo wa Diamond aliieleza mahakama kuwa kutokana na muda kwenda amefanya mawasiliano na Meneja wake Babu Tale na kwamba watalifanyia kazi suala hilo na kuliweka sawa.
Kwa upande wa wakili wa Wandwi, Felix Buruda ameielezea Mahakama kuwa, wakili wa mlalamikiwaji Diamond maelezo yake ni mbinu ya kupoteza muda wangeweza kuwasiliana naye kwa njia ya barua pepe ili aweke mambo sawa.
Wakili wa Diamond kutokana na kuendelea kuieleza Mahakama kuhusu kesi hiyo, alikuwa anaeleza vitu tofauti na alichoandika kwenye maelezo ya utetezi wa mlalamikiwaji hadi kufikia Hakimu Laurent Wambili ambaye alikuwa muendesha mashitaka kutoa saa mbili pande zote mbili zijadiliane ili Mahakama iweze kuendesha kesi kwa urahisi.
No comments:
Post a Comment