Mkurugenzi Mkuu wa NIC Bank, Margret Karume (kushoto) akimkabidhi vifaa
mbalimbali Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi kwa
ajili ya wagonjwa wa Fistula waliolazwa kwenye hospitali hiyo ikiwa ni sehemu
ya kusherehekea kwa pamoja maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani. Hafla hiyo
imefanyika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi akiongea na waandishi wa habari kutoa shukrani zake kwa Benki ya NIC mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa wa
Fistula waliolazwa kwenye hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea kwa
pamoja maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani. Hafla hiyo imefanyika Hospitali
ya CCBRT jijini Dar es Salaam.
Meneja Chapa
na Mawasiliano wa NIC Benki, Bi Nasikiwa Berya
akiongea kabla kukabidhi vifaa mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa wa Fistula waliolazwa kwenye hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea kwa pamoja maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani. Hafla hiyo imefanyika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa NIC Bank, Margret Karume (kushoto) akisikiliza taarifa mbali mbali kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT (hayupo pichani).
Na Mwandishi Wetu
Ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Kimataifa ya
Wanawake Duniani, Benki ya NIC imeadhimisha siku hiyo muhimu kwa wanawake kwa
kutembelea na kutoa misaada mbali mbali kwa wanawake wanaotibiwa ugonjwa wa
Fistula hospitali ya CCBRT.
Siku ya Kimataifa ya Wanawake huazimishhwa kila mwaka
kusherehekea mafanikio waliyopata wanawake katika nyanja mbali mbali kama vile
kijamii, kiuchumi, kitamaduni na kisiasa.
Maadhimisho haya pia yanasaidia kupaza sauti juu ya
suala la usawa wa kijinsia. Yakiwa na kauli mbiu ‘Usawa kwa Wote’, kauli hiyo
inahimiza kuwa usawa siyo jambo la wanawake bali ni jambo la kibiashara. Usawa
wa kijinsia ni muhimu kwa uchumi na kwa maendeleo ya jamii. Usawa wa kijinsia
siyo jambo la mjadala wa siku moja ambao utaisha katika siku ya wanawake duniani
bali ni suala endelevu.
Ili kusaidia jamii ambayo inatuzunguka, tumeamua
kutumia siku hii kuimarisha uhusiano wet na hospitali ya CCBR. Benki yetu leo
imeamua kuja hapa na kutoa misaada mbali mbali itakayowasidia wanawake wanopata
matibau ya fistula hospitalini hapa,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo
Margaret Karume.
Akizunguma wakati wa kutoa misaada hiyo, mkurugenzi wa
benki hiyo alisema benki yake ni moja kati ya taasisi zinazojali suala la usawa
i kwenye mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na ajira na kuongeza kuwa pia benki
hiyo inathmini jamii inayozizunguka na huzisadia katika nyanja za elimu, afya
na mazingira.
“Tunafurahi kushiriki maadhimisho ya siku ya wanawake
duniani pamoja wanawake hapa CCBRT. Kusaidia jamii inayotuzunguka na wanawake
ni moja kati ya vipaumbele vya benki yetu.
Unapomsaidia mwanamke, humsaidii peke yake bali
unasaidia jamii nzima nan chi kwa ujumla,” alisema Usawa wa kijinsia unahitaji
uwezeshaji kwa wote ukilenga kutatua changamoto ya kutokuwa na maamuzi sawa na
pia kumpa kila mtu nguvu na uhuru wa kuamua maisha yake.
Aliongeza kuwa watu wote wakiwa wamewezeshwa, familia
zinanufaika na manufaa haya yanakwenda mpaka kwa vizazi vijavyo na familia kwa
ujumla.
Benki ya NIC itaendelea kusaidia jamii katika namna
mbali mbali ambazo zitamnufaisha mtu mmoja mmoja na jamii yote kwa ujumla
wake,” alisema.
No comments:
Post a Comment