A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, March 18, 2020

BENKI YA CRDB YAZINDUA MPANGO MAALUM WA KUTOA MAONI KWA NJIA YA "QR CODE"

Benki ya CRDB imezindua mpango maalumu wa kuwasilisha maoni ya mteja kwa njia ya QR Code. Akizindua mpango huo Mkurugenzi wa Mawasiliano wa benki hiyo, Tully Esther Mwambapa alisema, Njia hiyo itamwezesha mteja kutoa maoni kwa Benki bila usumbufu wowote na kwa muda mfupi sana.

"Anachotakiwa kufanya mteja ni kuscan kwenye QR Code kwa kutumia simu yake ya smart ambayo imeunganishwa na internet, Mteja atafungua camera ya simu yake na kuscan kwenye QR Code ambazo zinapatikana kwenye matawi yote ya Benki halafu itampeleka moja kwa moja kwenye website ya CRDB Bank, huko atakutana na maswali ambayo yatamwongoza kwenye kutoa maoni; ikiwa, kuona listi ya Matawi yote ya Banki ambayo atatakiwa kuchagua tawi ambalo anahitaji kulitolea maoni na baada ya hapo atatuma amoni yake. Maoni hayo yatakwenda moja kwa moja kwenye kitengo husika cha Benki ya CRDB na kufanyiwa kazi".

Aidha Mkurugenzi wa Mawasiliano amewataka wateja kutumia huduma hii kuwasilisha maoni yao ambayo kwa namna moja yatasaidia kuboresha huduma za kibenki na kuendelea kuwahudumia wateja wake kwa weledi mkubwa zaidi bila wasiwasi.

Uzinduzi wa mpango huo wa kutoa maoni, umeanza kutumiwa na Matawi matano ya jijini la Dar es salaam na baadaye huduma hiyo itapatikana kwenye matawi na mawakala wote wa Benki hiyo nchi nzima.


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (katikati) akinguzumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango maalumu wa kuwasilisha maoni ya mteja kwa njia ya QR Code, wakati wa uzinduzi wa mpango huo uliofanyika kwenye Tawi la Benki ya CRDB, Mlimani City jijini Dar es salaam, Machi 17, 2020. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Urio na kushoto ni Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Pwani, George Yatera.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (kushoto) akionyesha namna ya kutumia mpango maalumu wa kuwasilisha maoni ya mteja kwa njia ya QR Code, wakati wa uzinduzi wa mpango huo uliofanyika kwenye Tawi la Benki ya CRDB, Mlimani City jijini Dar es salaam, Machi 17, 2020. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Urio na kushuhudiwa na wafanyakazi wengine wa Benki hiyo. Huduma hiyo imezinduliwa kwa kuanza na Matawi matano ya jijini la Dar es salaam na baadaye huduma hiyo itapatikana kwenye matawi na mawakala wote wa Benki hiyo nchi nzima.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (wa pili kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Urio (kulia) wakimuelekeza mmoja wa wateja wa Benki ya CRDB, namna ya kutumia mpango maalumu wa kuwasilisha maoni ya mteja kwa njia ya QR Code, wakati wa uzinduzi wa mpango huo uliofanyika kwenye Tawi la Benki ya CRDB, Mlimani City jijini Dar es salaam, Machi 17, 2020. Huduma hiyo imezinduliwa kwa kuanza na Matawi matano ya jijini la Dar es salaam na baadaye huduma hiyo itapatikana kwenye matawi na mawakala wote wa Benki hiyo nchi nzima. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Matawi wa Benki ya CRDB, Bonventura Paul.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (kushoto) akiwa pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Urio (kulia) wakimuelekeza mmoja wa wateja wa Benki ya CRDB, Beatrice Bariki namna ya kutumia mpango maalumu wa kuwasilisha maoni ya mteja kwa njia ya QR Code, wakati wa uzinduzi wa mpango huo uliofanyika kwenye Tawi la Benki ya CRDB, Mlimani City jijini Dar es salaam, Machi 17, 2020.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es salaam wakionyesha namna ya kutumia mpango maalumu wa kuwasilisha maoni ya mteja kwa njia ya QR Code, wakati wa uzinduzi wa mpango huo. 
Picha ya pamoja.







No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages