A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, December 19, 2019

BENKI YA NMB YATAMBULIWA KUWA MWAJIRI ALIYEIDHINISHWA NA CHAMA CHA WAHASIBU ULIMWENGUNI (ACCA)

Benki ya NMB imepokea kibali cha ithibati kuwa mwajiri aliyeidhinishwa na Chama cha Wahasibu cha Kimataifa Association of Chartered Certified Accountants (ACCA) katika kutoa maendeleo stahiki ya taaluma kwa wafanyakazi.

Utambuzi huu unamaanisha kwamba Benki ya NMB ina kiwango cha kimataifa cha kutoa fursa za wafanyakazi kujiendeleza kitaaluma na kuamini kuwa mafunzo hayo husaidia wanachama wa ACCA kwenye benki na taaluma nyingine kukidhi mahitaji yao ya uzoefu wa vitendo makazini.

NMB walipokea utambuzi huo kutoka ACCA mwishoni wa mwaka huu, ambapo NMB inakuwa miongoni mwa taasisi 13 nchini na taasisi za kimataifa zisizopungua 7,000 duniani zinazotambuliwa na ACCA.

NMB na ACCA zitaendelea kuhakikisha wafanyakazi wanakuzwa kwa viwango vya juu zaidi. Ambapo NMB itaendeleza kuweka mazingira mazuri na rafikii ya kufanya kazi ili kusaidia wanachama na wanafunzi wa mafunzo ya ACCA kupata mafunzo stahiki.

Akizungumza katika mahojiano maalumu, Meneja mwandamizi Idara ya Ukaguzi wa ndani NMB, Gaudence Nganyagwa, amesema ni wakati sasa wa Tanzania na Ulimwengu kufahamu jinsi gani NMB inathamini wafanyakazi wake kwa kuwajengea uwezo ili kuwa wenye ushindani katika kutoa huduma bora yenye weledi wa kimataifa.

“Tunaamini kuwa ni wakati wa kuifanya Tanzania na Ulimwengu ujue ni kwa kiasi gani NMB tunathamini maendeleo ya wafanyakazi wetu. Kwa miaka mingi, benki imekuwa ikiwekeza katika mafunzo na kuwaendeleza wafanyakazi ili kuzalisha kilicho bora sokoni.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages