MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo amewakaribisha watendaji wa kata zote nchini Katika Jiji la Dar es Salaam, huku akiwahakikishia usalama wanapokuwa hapa tangu Septemba 2 mwaka huu kwa ajili ya mkutano uliondaliwa na Rais John Magufuli.
Rc Makonda ameyasema hayo alipofanya mkutano na wanahabari akielezea kufurahishwa kwake na ujio huo kuwa ni fursa kubwa kwa wafanyabiashara na wananchi wake ambapo mkutano huo utaongeza wigo wa biashara sehemu mbalimbali na kwamba hawatakumbana na kero za wezi katika jiji hilo.
"Ugeni huu katika mkoa wangu ni sehemu yake ya utaratibu ambao Rais wa awamu ya tano amejiwekea,ikiwemo kuzungumza na makundi mbali mbali ikiwemo viongozi wa dini msishangae akawaita Wenyeviti wa serikali ya Mitaa ili ajue changamoto zao "alisema Makonda.
Amewataka wafanyabiashara kutumia nafasi hiyo kufanya biashara mbali mbali kwa dhumuni la kuutangaza mkoa wetu ambapo amewataka watendaji hao wanapofika Katika jiji Hilo waweze kutalii na kufurahia kufika Katika mko huo.
"Tukio la Rais kuwaita Watendaji Ni Jambo jema kwani anawapa fursa watendaji kuwa Pamoja na kufahamishana Mambo mbalimbali Katika utendaji na hili si Jambo la kisiasa hivyo tuache kuingiza kazi na siasa watendaji ni watumishi wa Serikali anawaita kwa ajili ya kuwapa moyo"Amesema Makonda.
Wakati huohuo Makonda amewataka wananchi kujenga tabia ya usafi kuanzia ngazi ya mtaa na kata,amewataka wenye nyumba barabarani kufunga taa Kila pande ili kusaidia usalama Pamoja na kumfanya mtu kuwa na hofu ya kuchafua mazingira.
No comments:
Post a Comment