TANZIA: Taarifa zilizotufikia ni kwamba mmoja wa wasanii wa Bongo Fleva wanaounda Kundi la The Mafik, aitwaye ‘Mbalamwezi‘ (pichani katikati) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Ijumaa, Agosti 15 2019.
Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na msanii mwenzake wa kundi hilo aitwaye Hamadai (pichani juu kushoto), lakini chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana.
Taarifa za awali kutoka kwa baadhi ya ndugu wa marehemu, zinasema mwili wake ulikutwa maeneo ya Africana Dar, ukiwa hauna nguo na ikiwa ni saa kadhaa zimepita tangu atokomee bila kujulikana alipo.
Mwili wa marehemu Mbalamwezi umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam.
Taarifa zaidi tunaendelea kukujuza.
No comments:
Post a Comment