Polisi ya Hong Kong imefyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya zaidi ya waandamanaji 1,000 ambao walilizuia lango kuu la kituo cha treni cha Tai Wai kilichopo katika wilaya ya Kowloon.
Idadi nyingine ya waandamanaji walizuia eneo la kuingilia la treni ya ardhini, ambayo inawabeba abiria wengi kuelekea bandari ya Hong kong.
Mapema leo, waandamanaji walianza kufanya mikusanyiko miwili, wakiipinga marufuku ya polisi, ambao wamekuwa wakikabiliana nao kwa takribani miezi miwili.
Maandamano hayo yana lengo la kuupinga mswada wa sheria ambao ungetoa mamlaka ya wakazi wa Hong Kong kwenda kushitakiwa China Bara na malalamiko mengine kuhusu serikali ya China.
No comments:
Post a Comment