Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini(REA), Katika Wilaya ya Bagamoyo na Chalinze Mkoni Pwani ambapo mradi huo utafanywa na Mkandarasi kutoka Kampuni ya SINOTEC.
Mbunge wa Jimbo la bagamoyo Shukuru Kawambwa, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini(REA), Katika Wilaya ya Bagamoyo na Chalinze Mkoni Pwani ambapo mradi huo utafanywa na Mkandarasi kutoka Kampuni ya SINOTEC
Baadhi ya viongozi waliohudhulia hafla ya uzinduzio huo
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu (wanne kushoto waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na wafanya kazi wa Shirika la umeme Tanesco Bagamoyo.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, akisalimiana na wakazi wa Chalinze waliohudhuria ufunguzi huo
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu (watatu kushoto waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali kulia kwa waziri ni Mbunge wa Jimbo la Chalize Ridhiwan Kikwete.
Mbunge wa Jimbo la Chalize Ridhiwan Kikwete (kulia), akisalimiana na Viongozi kutoka Kampuni ya SINOTEC wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, ya uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini(REA), Katika Wilaya ya Bagamoyo na Chalinze Mkoni Pwani ambapo mradi huo utafanywa na Mkandarasi kutoka Kampuni ya SINOTEC.ya
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, amewataka Meneja Tanesko
kote nchini kuwa
wabunifu Katika kutatua
changamoto za kukatika kwa umeme na kuhakikisha umeme unakuwa wa uhakika.
Naibu Waziri wa Nishati ameyasema hayo Katika uzinduzi wa
Mradi wa Umeme Vijijini(REA), Katika Wilaya ya Bagamoyo na Chalinze Mkoni Pwani
ambapo mradi huo utafanywa na Mkandarasi
kutoka Kampuni ya SINOTEC.
" Tunataka umeme unaosambazwa uwe wa uhakika kutokana na
Juhudi za Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli za kupatikana kwa
Nishati hasa vijijini naomba Sana Mameneja nchi nzima muwe wabunifu wa kutatua
matatizo ya kukatika kwa umeme" Amesema Naibu Waziri.
Amesema Mradi huo utasaidia kupunguza changamoto za miradi
ambapo umeme huu utawaka maeneo mbalimbali ikiwemo Shule, hospitali, sehemu za
ujasiriamali Pamoja na makazi ya watu.
Aidha amewataka kampuni hiyo ya SINOTEC kuhakikisha wanafanya
Kazi kwa wakati amabapo watafanya Kazi ndani ya miezi Tisa.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la bagamoyo Shukuru Kawambwa
ameipongeza wizara ya Nishati kwa kuhakikisha Nishati inapatikana Katika
Vijijini.
Amesema umeme huo utawasaidia wakazi wa Bagamoyo kupata umeme wa
uhakika, na kuwataka kampuni iliyopewa dhamana ya kufanya Kazi hiyo kuifanya
kikamilifu na kwa uhakika.
Fedha zilizotengwa kwa ajili ya kukamilisha Mradi wa Peri Urban
Ni shilingi billion 12, na million 880.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa SINOTEC kwa ukanda wa Afrika Jin
Hua, ameishukuru Serikali ya Awamu ya tano kwakuiami ni SINOTEC na ameahidi kuwa anafanya kazi hiyo kwa muda uliopangwa.
SINOTEC nikampini iliyofanya miradi kadhaa hapa nchini hivyo
wanauzoefu mkubwa na imejiwekea uwaminifu
na historia nzuri katika kazi
walizofanya hapa nchini.
MATUKIO KATIKA PICHA
No comments:
Post a Comment