Kampuni ya basi la Safari Njema limegongana na Lori la kampuni ya Tumbaku Alliance usiku wa kuamkia leo ambapo watu wanne wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Wilbroad Mutafungwa amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi ambalo lilikuwa linatoka Dar es salaam kwenda Dodoma kutaka kulipita gari la mbele yake bila kuchukua tahadhari.
Kamanda Mutafungwa alisema "Akiwa ana overtake bila kuchukua tahadhari akagongana na gari lililokuwa mbele yake kwa ubavu, bahati mbaya watu wanne wamepoteza maisha.”
Ajali hiyo imetokea eneo la Nanenane katika Manispaa ya mkoa wa Morogoro nchini Tanzania ambapo dereva wa basi ametoroka na Jeshi la polisi likiendelea kumtafuta.
Majeruhi waliokuwa kwenye basi walipelekwa hospitali kwa sababu ya kupata mshtuko na baadhi yao wameruhusiwa kuondoka na wengine watatu wanaendelea kupata matibabu.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Friday, August 16, 2019
Tags
LOCAL#
Share This
About kilole mzee
LOCAL
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment