CHUO Kikuu cha Afya na Tiba cha St.Joseph jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na wanafunzi wanatarajia kukusanya damu lita 100 kwa ajali ya kusaidia majeruhi wa ajali ya mafuta iliyotokea Agasti 9 mwaka huu mkoani Morogoro.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uchangiaji wa damu Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo hicho Joackim Ndali amesema kuwa wameguswa na ajali hiyo na kuona kama wanafunzi wanaweza kutoa msaada wa kuokoa majeruhi waliolazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ya jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa katika moyo huo watu wengin zikiwmo taasisi zijitokeze katika uchangiaji wa damu na kuwa ni sehemu ya maisha ya kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wenye uhitaji wa damu.
Ndali amesema kuwa kama chuo katika uchamgiaji wa damu wananfunzi wamejitoa kutokana na kuguswa na majeruhi ya ajali ya mafuta mkoani Morogoro.
Nae Mwanafunzi wa Chuo hicho elisafi Elibariki amesema kuwa kuna uhitaji wa damu nyingi licha ya kuwepo kwa majeruhi hao wapo watu wengine wa ajali pamoja na wazazi wakati wa kujifungua.
Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Tiba cha ST Joseph Joackim Ndali akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uchangiaji damu kwa ajili ya majeruhi wa ajali ya mafuta mkoani Morogoro waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa Chuo hicho elisafi Elibariki akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana umuhimu wa uchangiaji damu wa wahitaji katika kuokoa maisha katika uchangiaji wa damu uliofanyika katika chuo hicho.
Mwanafunzi akichangia damu kwa ajili ya majeruhi wa ajali ya mafuta mkoani Morogoro waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi na wahadhiri wakiwa katika maandalizi ya uchangiaji damu.
No comments:
Post a Comment