Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya bima Sanlam kanda ya Afrika Mashariki, Julius Magabe wakishikana
mikono baada ya kufungua pazia la jiwe la msingi katika uzinduzi wa madarasa
mawili na ofisi ya walimu ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa
msaada wa Kampuni ya Bima ya Sanlam kwa thamani ya shilingi Milioni 49.
Uzinduzi huo ulifanyika shuleni hapo tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa, Mkoani
Dodoma mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life, Khamis
Suleiman , Kamishna wa
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Dk. Mussa Juma (wa pili kulia) na Meneja
wa Mamlaka hiyo kanda ya kati, Stella Rutaguza (kulia).
Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (kushoto) akipeana mikono na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Bima Sanlam kanda ya Afrika Mashariki, Julius Magabe
wakati wa hafla ya makabidhiano ya madarasa mawili na ofisi ya walimu ya
Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bima Sanlam kwa
thamani ya shilingi Milioni 49. Uzinduzi huo ulifanyika shuleni hapo tarafa ya
Pahi, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Katikati ni Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima
(TIRA), DK. Mussa Juma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.
Ashatu Kijaji (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima Sanlam Kanda
ya Afrika Mashariki, Julius Magabe wakifungua pazia la jiwe la msingi
kuzindua madarasa mawili na ofisi ya walimu ya Shule ya
Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bima ya Sanlam yenye
thamani ya shilingi Milioni 49. Uzinduzi huo ulifanyika shuleni hapo tarafa ya
Pahi, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Kutoka Kushoto ni
Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya Bima ya Sanlam Life, Khamis Suleiman , Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Dk.
Mussa Juma na Meneja wa Mamlaka hiyo Kanda ya Kati, Stella Rutaguza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima
ya Sanlam Kanda ya Afrika Mashariki, Julius Magabe, akizungumza katika hafla ya
makabidhiano ya madarasa mawili na Ofisi ya walimu ya Shule ya
Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bima Sanlam kwa gharama ya
shilingi Milioni 49. Makabidhiano yalifanyika shuleni hapo, Pahi, Kondoa,
Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango, Dk. Ashatu Kijaji na Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Dk. Mussa Juma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.
Ashatu Kijaji akihutubia
katika hafla ya uzinduzi
pamoja na makabidhiano ya madarasa mawili na ofisi ya walimu ya Shule ya
Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bima ya Sanlam kwa
gharama ya shilingi Milioni 49. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo, tarafa ya
Pahi, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya
Sanlam Life, Khamis Suleiman akihutubia katika hafla ya uzinduzi pamoja na makabidhiano ya madarasa
mawili na ofisi ya walimu ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa
kwa msaada wa Sanlam kwa gharama ya shilingi Milioni 49. Hafla hiyo ilifanyika
shuleni hapo, tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma mwishoni mwa
wiki. Katikati waliokaa ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Ashatu Kijaji
na kushoto kwake ni Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Dk. Mussa Juma.
Watanzania hawana budi kuchukulia bima kama
hitaji muhimu na kujifunza aina mbalimbali za bidhaa za bima zilizopo sokoni
ili wazitumie kujikinga, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Ashatu Kijaji amesema
hivi karibuni akiwa ziarani wilayani Kondoa, Mkoani Dodoma.
Waziri huyo alitoa wito huo wakati wa hafla ya
uzinduzi na makabidhiano ya madarasa mawili, ofisi ya walimu na madawati 40
vyenye thamani ya jumla ya Tsh 49m kwa shule ya Msingi Lusangi iliyopo wilayani
Kondoa, vilivyojengwa kwa msaada wa kampuni ya bima ya Sanlum, ambayo ndiyo
mtoaji mkubwa wa bima barani Afrika.
“ Huduma ya bima inahitajika sana ili
kuwawezesha watu kujikinga na majanga yasiyotabirika ya siku za usoni,” alisema
Dr. Kijaji, na kuongeza kuwa ishara iliyoonyeshwa na kampuni ya Sanlam ya kurudisha
sehemu ya faida yake kusaidia miradi ya jamii ichukuliwe kama ishara
ya namna gani bima ni muhimu kwa uhakika wa maisha.
Akiongea katika hafla hiyo,
Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda – Afrika Mashariki wa Sanlam Pan-Afrika, Julius
Magabe, alisema kampuni hiyo itaendelea kusaidia miradi ya jamii nchini
Tanzania.
“ Naomba nichukue fursa hii
kuwahakikishia kuwa Sanlam tutaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania
katika kutoa fedha kwa miradi mbalimbali ya jamii”, alisema Magabe, nakuongeza
kuwa kampuni hiyo – ambayo imesherehekea mwaka 2018 imesherehekea miaka 100
tangu kuanziswha kwake, iko thabiti katika kurejesha sehemu ya faida yake
kusaidia jamii.
Awali akiongea katika hafla hiyo, Mwalimu Mkuu
wa Shule ya Msingi Lusangi, Josephine Paul, alisema shule hiyo ilikuwa
inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madarasa, kwa kuwa madarasa matano
yaliyokuwepo kabla hayakuweza kutosheleza idadi ya wanafunzi ambayo ni 348.
“Kutokana na mradi huu kukamilika, utakuwa
umepunguza changamoto ya upungufu wa madarasa na oofoso ya walimu uliokuwepo,”
alisema mkuu huyo wa shule.
Na katika hali ya kuonyesha ufanisi nadra
katika matumizi ya fedha za wafadhili kitendo ambacho kilimvutia waziri Dr.
Kijaji na vilevile ujumbe wa Sanlam, ujenzi huo siyo tu ulikamilika ndani ya
muda uliopangwa, bali zaidi ya Tsh 2.7m zimeokolewwa kutokana na kupunguza
gharama, fedha ambazo zimewekezwa katika ujenzi wa vyoo wa wanafunzi wa kike na
wa kiume.
“ Sisi Sanlam hatujawahi kushuhudia
mradi tunaoufadhili ukisimamiwa kwa umakini wa hali ya juu kiasi hiki,” Alisema
Magabe, ambayo kampuni anayotumikia ina matawi ndani ya nchi 38 barani Africa,
huku huduma zake zikiwa zimesambaa mabara ya Amerika, Asia na Australia
No comments:
Post a Comment