NA HERI SHAABAN
MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema kwamba Wakazi wa kata ya Jangwani watakuwa chini ya uangalizi kwa lengo la kuwaepusha na magojwa ya mlipuko Dengue na Kipindupindu.
Mjema ameyasema hayo leo, wakati wa kufanya usafi wa Mazingira uliyofanyika Wilaya ya Ilala sambamba na upulizaji wa Dawa za Dengue na Kipindupindu kata za Mchikichini na Jangwani Manispaa ya Ilala.
"Ndani ya Wilaya yangu leo tumefanya usafi wa mazingira na kupuliza dawa ya kwa dhumuni la kuwakinga wananchi usafi ni muhimu ,akuna miujiza ukiona mgonjwa anatapika mpekeke hospitali, alisema Mjema
Mjema ameagiza kila mwananchi wa Wilaya ya Ilala kuweka maeneo yao safi,wale wakaidi katika suala zima la usafi kupigwe faini .
Amewataka kila jumamosi ngazi ya familia kufanya usafi katika maeneo yao kila mmoja kuakikisha maeneo yanakuwa safi.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Dkt.Emlly Lihawa amewataka wananchi kuchemsha maji ya kunywa ,kunawa mikono kila wakati kwa ajili ya kujikinga na magonjwa mbalimbali.
Aidha Dkt.Lihawa amewataka wananchi wa manispaa ya Ilala kutumia maji safi na salama kila wakati.
Almesema dawa hizo zilizopuliziwa katika kata hizo kwa ajili ya kuuwa mazalio ya mbuu na vimelea vya wadudu mbalimbali.
No comments:
Post a Comment