Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mheshimiwa Stella Ikupa amesema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni Mheshimiwa Maulid Mtulia aliyetaka kujua kama serikali inaweza kuorodhesha idadi ya walemavu nchini kwa kuzingatia makundi yao kwa asilimia.
Mhe. Ikupa amesema kwa mujibu taarifa ya Sensa ya Taifa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyotolea na Ofisi ya Taifa ya Takwimu idadi ya walemavu kwa makundi yaani Ualibino, Kuona, Usikuvu, Kutembea, Kukumbuka, Kujihudumia na Ulemavu mwingine ni milioni mbili laki sita elfu arobaini na moja mia nane na wawili na kwamba katika kuhakisha watu wote wenye ulemavu hasa vijana, watoto,na wanawake hawachiwi nyuma kiuchumi.
Amesema serikali inaendelea kuwajengea uwezo watoto wote wenye ulemavu ikiwa ni pamoja kuwapatia elimu na mafunzo ya ufundi stadi kwa makundi ya vijana na wanawake wenye ulemavu kupitia vyuo vya watu wenye ulemavu na program ya kukuza ujuzi hapa nchini.
No comments:
Post a Comment