A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, April 17, 2019

PROF. KABUDI AFUNGUA RASMI OFISI ZA UBALOZI WA CHINA JIJINI DODOMA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa Ofisi za Ubalozi wa China jijini Dodoma. Ufunguzi wa ofisi hizo umefanyika tarehe 12 Aprili 2019 na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Joseph Kakunda, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri anayeshughulikia uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki, Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Mussa Azan Zungu, Mzee Job Lusinde na Meya wa Jiji la Dodoma, Mhe. Prof. Davis Mwamfupe. Katika hotuba yake, Mhe. Prof. Kabudi ameupongeza Ubalozi wa China hapa nchini kwa uamuzi wa kufungua ofisi hizo na kuwataka wakazi wa Dodoma na wananchi kwa ujumla kuzitumia ofisi hizo kwa ajili ya kujiimarisha kibiashara na uwekezaji. 
Sehemu ya viongozi waliohudhuria ufunguzi wa Ofisi za Ubalozi wa China jijini Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) alipohutubia hafla hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akitoa hotuba yake. 
Sehemu ya wageni waalikwa nao wakifuatilia hotuba ya Prof. Kabudi (hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa Ofisi za Ubalozi wa China jijini Dodoma. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Caesar Waitara na kushoto ni Bw. Charles Mbando, Katibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Sehemu ya ujumbe wa China wakifuatilia hotuba ya Mhe. Prof. Kabudi (hayupo pichani).
Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke akizungumza wakati wa ufunguzi wa Ofisi za Ubalozi huo jijini Dodoma. Mhe. Wang Ke alisema kuwa ufunguzi wa Ofisi hizo ni kuunga mkono kwa dhati mpango wa Serikali ya Tanzania wa kuhamia makao makuu ya nchi uliotangazwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bofya hapa kwa picha zaidi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages