A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, April 19, 2019

Maneno yalizuka kuwa mimi ndio sababu ya kifo cha Ruge - Zamaradi

Mtangazaji,  Zamaradi ambaye ni mama watoto wa Ruge amesema kuwa kuna maneno yalizuka kuwa yeye ndio sababu ya kifo cha Aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji, Clouds Media, Ruge Mutahaba.

Zamaradi amesema kuwa mwanzoni alipokuwa akisikia maneno hayo alikuwa anakasirika lakini baadae akasema anakasirika nini na huenda ameacha alama kwa yule mtu.

"Ni sawa hata kuna maneno yalizuka kuwa am the reason ya kifo cha Ruge lakini mwanzo nilikuwa nakasirika lakini baadae nikasema nakasirika nini, nikasema huenda kuna alama fulani nimeiacha kwa yule mtu na ndio maana ambapo pale nilipoamua kukaa pembeni bado watu watanihusisha nae kwa namna yoyote kuna kitu kikubwa nilikiacha kwasababu najiuliza nimemuua mimi nini," alisema Zamaradi.

"I believe kuwa Ruge alikuwa ni mtu mzima baada ya kuachana na mimi alipita pita kidogo kwahiyo unataka kuniambia kote alikopita pita hakuna aliyewahi kumsahaulisha mimi, mimi tu ndio nimebaki ananiwaza tu mpaka leo kiasi kwamba anakuwa dipressed."

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages