A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, April 25, 2019

Hakuna mtu muongo kama CAG - Waziri Lugola


Waziri wa Mambo ya Ndani,  Lugola amesema hakuna mtu muongo kama CAG na kwamba yupo tayari kuweka uwaziri wake rehani.

Amesema hayo leo Bungeni kwa kueleza ikiwaitabainika kuwa taarifa zake za ukaguzi kuhusu sare hewa za jeshi la polisi zilizogharimu Tsh. Bilioni16 ni ya kweli.

“Sijawahi kuona mtu muongo kama CAG, Jeshi la Polisi hakuna sare hewa. Ninaomba maofisa wa ofisi ya CAG twende nao stoo wakaone sare mpya za jeshi la polisi. Kama nasema uongo nitajivua nguo na ninaweka uwaziri wangu rehani,” amesema.

Hivi karibuni Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof Mussa Assad  alishawasilisha ripoti ya ukaguzi wa hesabu kwa mwaka 2017/18 ndipo akaibua hayo. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages