A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, April 23, 2019

DC Iringa akanusha uwepo wa kiwanda cha kutengeneza Uume Bandia


Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela ametoa ufafanuzi mara baada ya kusambaa kwa picha zinazomuonesha  akiwa ameshika viungo bandia vya kiume na kuzua Taharuki katika jamii.

Akizungumza na Wandishi wa habari ofisini kwake leo Kasesela amesema kuwa taarifa zilizosambaa mtandaoni juu ya uzalishaji wa viungo bandia vya kiume, zimeleta changamoto huku akiwataka wananchi  kuondokana na dhana potofu za kuchukua habari za mitandaoni na kuupotosha umma.

“Naomba niendee kuwaomba radhi watanzania kwa ajili ya jambo ambalo lilileta taharuki kwenye mitandao ya kijamii hasa nchi ya jirani zetu hapo Kenya lilipokelewa tofauti na nilivyokuwa
hapo awali” alisema Kasesela.

Kasesela aliwataka watanzania kuacha kufuatia mambo ya ajabu na kuyapa nafasi kwenye mitandao ya kijamii kuliko kupata mambo ya kujenga nchi na yenye tija.

Aliendelea kwa kusema, 'Jamni ile habari ilitungwa na ni habari ya hovyo sana kwa kuwa nililishwa habari ambayo mimi sijaisema kwenye chombo chochote kile kwenye vyombo vya habari hivyo hiyo habari ni yakupuuza tu. Kwa sasa habari nyingi ambazo zinazungumzwa hivi sasa ni habari ambazo ni za hovyo hovyo mno ndio maana leo wamesema kuwa wilaya ya Iringa kuna kiwanda hicho kitu ambacho sio kweli'

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages