A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, February 20, 2019

SMZ yatoa ufafanuzi kuhusu Madaktari wanaofanya kazi Serikalini na vituo binafsi


Na Thabit Madai.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetoa Ufanuzi juu ya Madaktari ambao wanafanya kazi katika Hospitali za Serikali na vituo binafsi.

Ambapo imesema hakuna tatizo ikiwa Madaktari hao watafanya kwa ufanisi na kufuata utaratibu wa kazi kisheria.

Ufafanuzi huo ulitolewa na Naibu Waziri wa Afya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Harusi Said Suleimani wakati akijibu swali la mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake Pemba (CCM), alietaka kujua utaratibu upo vipi kwa madaktari wanaofanya kazi serikalini na katika vituo vya binafsi.

Akijibu swali la mwakilishi huyo Naibu Waziri huyo alisema mkataba wa kazi unamtaka Daktari afanye kazi kwa ufanisi kwa muda alopangiwa badala ya mda wake kuisha anaruhusiwa kufanya kazi za ziada.

Alisema taasisi mbali mbali Wafanyakazi wake hutumia muda wa mapumziko kwa kufanya kazi ya ziada katika sekta mbalimbali ili mfanya kazi aweze kujiongezea kipato cha kujikimu na Maisha.

Aidha Naibu Harusi alitumia fursa hiyo kuwataka wafanyakazi wa Wizara yake kufanya kazi kwa ufanisi ili kuweza kuwasaidia Wagonjwa pamoja na kuepuka kukiuka Sheria na maadili ya kazi.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages