Baadhi ya
washiriki wa jukwaa la Founder 2 Founder iliyoandliwa na SmartLab
wakifurahia kupata selfi ya kumbukumbu baada ya kongamano kuisha
SmartLab yafanya mkutano wa 3 wa
wavumbuzi uitwao Mwanzilishi kwa Waanzilishi
Smartlab
leo imefanya awamu ya tatu ya mfululizo wao wa Mwanzilishi kwa Waanzilishi
katika ofisi za Seedspace, Victoria, Dar es Salaam Tanzania kualamisha mwanzo
wa matukio yao waliyopanga kwa mwaka 2019.
Smartlab
imekua ikileta pamoja watu wa umuhimu kwenye sekta ya uvumbuzi kwa jioni za
maongezi na kufundishana miongoni mwa hao waanzilishi. Wanafanya hivyo kupitia
majadiliano kwenye mada tofauti tofauti ili kupata ufahamu wa jinsi ya kukuza
kampuni mpya. Tukio lilikua na mandhari ya “Jinsi ya kukuza kiufanisi soko la kampuni
yako mpya” na ilikua na jopo la watu kutoka sekta tofauti.
Mwanzilishi
kwa Waanzilishi ni jukwa kwa ajili ya kampuni mpya kukutana na wawekezaji,
waanzilishi wenza na washirika. Na inawawezesha kuungana na kushirikiana wakati
wanbadilishana mawazo ya ubunifu kwa ajili ya kukua, kubadilisha mitazamo na
kutengeneza ufumbuzi wa kubadilisha mazingira ya Tanzania na Africa kwa ujumla.
Akiongea
kwenye tukio, Edwin Bruno, Mwanzilishi wa SmartLab na mkurugenzi mtendaji wa
Smart codes Limited alisema kwamba “Kampuni mpya, wajasiriamali, wabunifu na
wavumbuzi wa biashara za hapa nyumbani sasa wana sehemu moja ya kukutana na
kufanya shuguli ambazo zitakutanisha na kukuza jumuiya za uvumbuzi zilizo
tofauti na zenye vipaji hapa Tanzania na africa kwa ujumla kupitia Mwanzilishi
kwa Waanzilishi”, Pia alieleza kua “Jukwaa la Mwanzilishi kwa Waanzilishi
linatoa muungano wa muhimu ambao unawezesha wajasiriamali na kampuni mpya kujua
mienendo mipya kwenye sekta ya uvumbuzi. Pia inawapa uwezo wa kujielezea kuhusu
changamoto zao na hivyo kutengeneza nafasi za suluhisho kwa ajili ya mapungufu
yao”.
Bwana Kumeil Abdulrasul, Bidhaa na
ushirikiano, Raha Liquid Telecom, mdhamini mkuu wa tukio aliongeza “Tunajivunia
kua sehemu ya tukio la SmartLab Mwanzilishi kwa Waanzilishi awamu ya tatu.
Ubunifu ndio hatima ya miaka ya mbele na Raha Liquid Telecom inajivunia kua
sehemu ya timu ambayo inataka kubadili hatima ya ubunifu, kampuni mpya na
mazingira ya ubunifu Tanzania”.
Smart Lab ni jukwaa la ubunifu linalo
unganisha taasisi za elimu na mashirika suluhisho mapya ambayo zitaleta athari
nzuri katika jumuiya za Africa.
No comments:
Post a Comment