A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, February 7, 2019

Naibu Waziri Shonza auzungumzia wimbo wa Rayvanny na Diamond

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amezungumzia wimbo mpya wa Rayvanny na Diamond uitwao Tetema.

Katika mahojiano na Wasafi TV amesema kuwa ni wimbo mzuri na mara kadhaa ameusikiliza, huku
akimpongeza Diamond kwa kazi nzuri.

"Ngoma yake nimeisikiliza inaitwa Tetema, yes, nimesikiliza ni wimbo mzuri. Diamond anafanya
vizuri, ni muimbaji mzuri, wimbo wote ni mzuri," amesema.

Wimbo Tetema umekuja mara baada ya ule Mwanza kufungiwa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kutokana na kukiuka maadili. Huu ni wimbo wa nne kwa wawili hao kufanya pamoja mara baada ya kuachia Salome, Iyena na Mwanza.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages