Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt.
Kebwe Stephen Kebwe akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mradi wa
Lishe Endelevu baada ya kikao kilichofanyika katika Hoteli ya Nashera
Mjini Morogoro. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Majura
Kasika, Meya wa Manispaa ya Morogoro Mhe. Pascal Kihanga, Mratibu wa
Mradi wa Lishe Endelevu Dkt. Joyce Kaganda na Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro Dkt. Frank Jacob
…………………….
Na Andrew Chimesela – Morogoro.
Imeelezwa kuwa tatizo sugu la
utapia mlo unaendelea kuwa tatizo hapa nchini kwa baadhi ya maeneo
unatokana na ukosefu wa Elimu inayopelekea watu wengi kuwa na utamaduni
wa kula vyakula vyenye viinilishe vya aina moja badala ya kula vyakula
vyenye mlinganyo wa virutubishi.
Kauli hiyo imetolewa Mwanzoni mwa
wiki hii na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe wakati wa
ufunguzi wa Kikao cha kutambulisha Mradi wa Lishe Endelevu
kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Nashela iliyopo Manispaa ya
Morogoro.
Dkt. Kebwe amesema watu wengi
wanapata chakula cha kutosha laikini kinachokosekana ni kukosa kula
chenye Chakula chenye mchanganyiko wa virutubishi vyote muhimu ukiwemo
Mkoa wa Morogoro ambao hauna tatizo la chakula ila watu kutokula vyakula
vyenye mlinganyo wa virutubishi.
“Kwa Mkoa wa morogoro chakula sio
tatizo, tatizo ni kutokula vyakula vyenye mlinganyo unaotokana na kukosa
wa Elimu”.Alisema Dkt. Kebwe.
Amesema Morogoro unachangia akiba
ya chakula hapa nchini kwa asilimia 30 na mchele wote unaoliwa na
watanzania asilimia 52 ya mchele huo unatoka Mkoa wa Morogoro, hivyo
amesisitiza kuwa Morogoro chakula sio tatizo, tatizo ni kutokuwa na
uelewa wa kula vyakula vyenye mlinganyo hivyo aameshauri Mradi wa Lishe
endelevu kutoa Elimu hiyo kwa nguvu zote.
Naye Mratibu wa Mradi wa Lishe Endelevu unaofadhiriwa na Watu wa Marekani kupitia Shirika la Save the Chidren Dkt.
Joyce Kaganda amesema takwimu za utapiamlo kitaifa zinaonesha unapungua
kwani 2010 kulikuwa na asilimia 42 ya utapia mlo, kwa sasa ni asilimia
34 na mpango wa Taifa wa maendeleo umedhamiria kupunguza utapia mlo hadi
kufikia asilimia 28.
Hata hivyo Dkt. Kaganda amesema
Mradi wa lishe endelevu kwa sasa utajikita katika kuhamasisha masuala ya
uratibu wa shughuli za Lishe Endelevu hapa nchini pamoja na kuweka
mipango ya kuongeza Bajeti ya utekelezaji wa shughuli za Lishe Endelevu
ikiwa ni pamoja na kutoa Elimu ya watu kubadili tabia kula vyakula
vyenye virutubishi vyote.
Kwa upande wa wajumbe walioshiriki
kikao hicho wakiwemo Wakuu wa Wilaya, na Wakurungenzi wa Halmashauri
huku Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe alisema ili kuweza
kufikia malengo ya mwaka 2020/2021 kuna haja ya wananchi kutumia vema
fursa ya maeneo yao kulima mazao yenye virutubishi vingi likiwemo zao la
viazi.
Huku Mkuu wa Wilaya ya Malinyi
Mhe. Majura amesema ili kujenga kizazi bora na chenye Afya ni vema Elimu
ikatolewa kwa jamii kuhusu malezi yanayotakiwa na vyakula vinavyotakiwa
kuliwa na mama Mjamzito tangu kutungwa mimba kwa mtoto, kulelewa hadi
kufikia siku elfu moja ambazo ni muhimu kwa mtoto.
Mradi wa Lishe Endelevu unaofadhiriwa na USAID kupitia Shirika la Save The Chidren
ni mradi wa miaka minne utakaotekelezwa kwa mikoa minne hapa nchini
ambapo kwa Mkoa wa Morogoro utatekelezwa kwa Halmashauri zote tisa za
Mkoa huo.
No comments:
Post a Comment