Na Mwandishi wetu, Mihambwe
Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amewashukuru Wazazi wa Wanafunzi Shule za Sekondari Tarafa ya Mihambwe kwa kuitikia vyema agizo la Serikali la kutaka Wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato Cha Kwanza kuwapeleka Shule.
Gavana Shilatu ameyasema hayo kwenye mahojiano ambapo ameeleza zoezi la kutoa elimu na hamasa limezaa matunda kwa ushirikiano na Watendaji kata, Watendaji Vijiji pamoja na uongozi wa Shule ndani ya Tarafa ya Mihambwe.
“Kwa muda mfupi niliyoanza ziara ya hamasa ya will wiki moja kuhakikisha Wazazi wanawapeleke Watoto wao Shule, Hali ya kuripoti shuleni imeongezeka kutoka asilimia 20.83 ya awali Hadi kufikia asilimia 66.8 iliyopo Sasa.
Nawashukuru sana Wazazi wote ndani ya Tarafa ya Mihambwe waliotii agizo la Serikali. Waliobakia nao pia wafanye hivyo kuwaleta Watoto shuleni.”Alisema Gavana Shilatu.
Gavana Shilatu kwa ushirikiano na uongozi wa Wilaya, Kata, Vijiji, Vitongoji na Shule amehaidi kuendelea kutia msukumo zaidi ili malengo ya kuripoti shuleni ya asilimia 100 yatimie.
No comments:
Post a Comment